Watu wamekuwa wakijiuliza kwa muda mrefu, maana/kirefu cha herufi S katika simu zinazotolewa na Samsung katika familia ya Galaxy S. Na sasa imejulikana huwa inamaana gani hasa.
Mtandao wa teknolojia wa Phonearena.com umefanikiwa kupata maana nzima baada ya kuona faili (document) ya siri kutoka Samsung.
Wakati makampuni mengine huwa wanachagua herufi za majina ya simu bila ya kuwa na maana yeyote kubwa chini yake fahamu kwa Samsung kuna maana kubwa ndani yake.
Maana ya “S” kumbe ni ‘Super Smart’, yaani ni ‘Janja Nzuri Sana’, au ‘Janja Babkubwa’.
– “S” (Super Smart) – Devices at the very pinnacle of Samsung’s mobile portfolio. This class will only be used on flagship devices such as the Samsung Galaxy S – Sehemu ya ‘document’ hiyo ilisomeka
Na pia simu za Samsung zinazotumia Galaxy Y ni kwa ajili ya vijana, tena hasa katika nchi zinazokua/zinazoendelea (kiuchumi). Galaxy W ni kwa ajili ya simu ambazo zina mvuto wa kitofauti pamoja na ubora mzuri kiutendaji.
Galaxy M (Magical) ni kwa ajili ya simu zenye uwezo mzuri na zilizowekwa kwenye bei zisizo kubwa sana.
Uamuzi wa kuleta matoleo ya Galaxy S ulikuwa ni moja ya maamuzi mazuri zaidi yaliyofanywa na kampuni hiyo kwani kwa miaka mingi mauzo ya simu za Galaxy S yamekuwa yakiwaletea mapato makubwa zaidi katika biashara yao.
Je ulikuwaga unajiuliza kwa muda mrefu kirefu/maana cha Galaxy S… sasa wajua 🙂
Source: PhoneArena
No Comment! Be the first one.