Mwaka 2017 ulikuwa ni mzuri sana kwa Google mara baada ya simu zake; Google Pixel 2 na 2 XL kununulika sana na kuifanya kampuni hiyo kuwa katika orodha ya kampuni ambzo bidhaa zake zilifanya vizuri mwaka huo.
Ni mwaka mwingine sasa na Google wapo mbioni kutoa toleo jingine la simu zake kutoka familia ya Pixel; hapa nikimaanisha Google Pixel 3 na 3 XL ambapo kwa taarifa zilizovuja zimeonyesha picha, sifa zake na hata lini zitazinduliwa.
Nini cha kutegemea kuona kwenye Google Pixel 3 na 3 XL?
Muonekano. Google Pixel 3 inasemekana kuwa intakuwa na umbo la mstatili mwanzo mpaka mwisho huku kioo chake kikiwa na urefu wa inchi 5.4. Kwenye Pixel 3 XL inategemewa kuwa na umbo la herufi “V” kwenye uso wa juu huku kioo chake kikiwa na urefu wa inchi 6.2.
Kamera. Simu zote mbili zimeonekana kuwa na kamera moja tu nyuma (kama ilvyo kwa watangulizi wake) lakini zikiwa na kamera mbili za mbele. Eneo la kamera ndio zilifanya toleo lililopita la Pixel kuwavutia wengi.
Uzinduzi wake. Bado haijafahamika lakini inaaminika simu hizozitazinduliwa Okt 4 2018 kama ilivyo kwa zile zilizopita ambapo zilitambulishwa tarehe na mwezi huo mwaka 2017.
Shauku ya wengi kutaka kujua uzuri/ubora wa Google Pixel 3 na 3 XL unatokana na toleo lililopita la simu hizo lakini itakumbana vikali na Samsung Galaxy Note 9.
TeknoKona itawaletea uchambuzi wa kina mara tu simu hizi zitakapokuwa zimetambulishwa rasmi kwa ulimwengu. Usiache kutufuatilia kila siku.
Vyanzo: Gadgets 360, Android Central