Uzuri na kinachovutia kwenye Instagram ni kuona machapisho ya picha/video kwenye Istagram ambapo itategemeana na watu uliowafuata.
Ni muda sana Instagram walikuwa wagumu kuboresha ambacho wengi walikuwa wnakilalamikia lakini sasa wahusika wamesikia na kuboresha kile ambacho hakikuwapendeza wengi.
Hapo awali ukifungua Instagram ulikuwa unaona machapisho ya mtu ya siku yoyote ile; kulikuwa hakuna mpangilio maalum lakini hilo sasa litabadulika kwani utaweza kuona machapisho ya mtu ambayo ni mpya ingawa sio katika mtiririko maalum.
Instagram yenye watumiaji zaidi ya milioni 800 kwa mwezi wamechukua takribani miaka miwili kuweza kuboresha yale ambayo yamelalamikiwa sana tena kwa muda mrefu. Kero nyingine ambayo imerekebishwa ni ule mtindo wa ‘Kuangalia kama kuna chochote kipya’ (refresh) bila ya wewe kutaka.
Sasa mtumiaji mwenyewe atachagua ni wakati gani wa app hiyo kurefresh na kama hatokuwa amebonyeza kitufe cha nyumbani ukurasa hautarefresh.

Instagram imesema itaendelea kuleta masasiho kwenye programu hiyo katika siku za usoni. Je, wewe una akaunti Instagram? Mambo haya mapya ni vitu ambavyo vilikuwa kero kwako kabla ya kuboreshwa?
Vyanzo: NYmag, Fortune
One Comment
Comments are closed.