Kwa sasa Pope Francis amejiweka tofauti na ma Pope wengine waliopita juu ya vitu vingi sana. Kwa mfano katoa sauti yake juu ya mambo mengi sana kama ndoa za jinsia moja na mabadiliko ya hali ya hewa.
Pope Francis pia inasemekana kuwa anataka kuweka rekodi ya kuwa Pope ambaye anapenda teknolojia kwa kuongezea katika akaunti yake ya Twitter amesema kuwa ataweza kuingia kwa mara ya kwanza katika mtandao wa kijamii unaohusisha picha na video yaani Instagram.
Kutokana na ripoti zilizopo ni kwamba akaunti hiyo itafunguliwa ifikapo machi 19 mwaka huu. Ripoti inaongezea kuwa Pope Francis atatumia jina la @Franciscus katika mtandao huo wa Instagram.
Pope Francis ambaye kwa kipindi cha mda mrefu amekuwa akisifu uwezo wa intaneti katika kukuza na kujenga jamii bora ambayo iko radhi ku’share’ mambo mbalimbali baina ya watu wake, amekuwa katika makutano ya siri na bwana Kevin Systrom, ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Instagram mwezi uliopita.
Hakuna ushahidi ambao unainyesha kuwa Bw. Kevin Systrom alimwalika Pope ilimradi tuu kutengeneza akaunti yake ya instagram. Lakini kutoka kwa akaunti ya Kevin ndani ya Instagram, waliongelea juu ya jinsi gani picha inaweza ikawa na uwezo mkubwa katika kuwaleta watu karibu duniani kote bila ya kujali mipaka kama vile lugha na tamaduni.
Ukiachana na utakatifu wake mwingi alionao bado Pope ana Followers Milioni 8.88 katika mtandao wake wa Twitter ambapo anatumia jina la @Pontifex ambapo alijiunga mwaka 2012. Na hapo bado ana akaunti zingine 8 ambazo ni ‘Official’ na zinatumia lugha tofauti tofauti zikijumuisha kitaliano, kifaransa na kiarabu.
Pope licha ya upendo wake katika Teknolojia pia ameshauri kuwa watu wasiwe wanatumia vifaa vyao wakati wa kula chakula. Na pia familia ambazo haziongei na kula pamoja ( katika Meza moja) hazihesabiki kama ni familia.