Vyombo vya usafiri tunavyotumia leo hii ni matokeo ya maendeleo ya kiteknolojia yaliyotokea katika kipindi cha miaka mingi ya matumizi, ubunifu wa vifaa vipya na uhitaji wa watumiaji. Katika makala hii tutaelezea kila chombo cha usafiri tangu kuanza kwake mpaka sasa kilipofikia.
Katika vyombo vyote vya usafiri Ndege ya abiria ndio chombo cha mwisho cha usafiri kutengenezwa na binadamu. Ambapo ndege ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1904.
Magari yamekuwa yakitumika kama chombo cha usafiri kwa zaidi ya miaka 100. Mpaka sasa kuna makampuni mengi duniani yanyotengeneza magari tofauti tofauti kulingana na aina ya soko wanalouzia. Aina hizi za magari ni pamoja na magari ya kifahari (Luxury cars), magari ya watendaji (SUV), magari ya mashindano (Sport cars) na aina zingine nyingi. Gari la kwanza lilitengenezwa mwaka 1886 na Carl Benz, Ujerumani.
Tofauti na magari ya zamani magari ya sasa yanauwezo wa kufungwa na kufunguliwa na rimoti, kujiendesha yenyewe, kutoa taarifa kwa dereve kama kuna shida yoyote kwenye gari na mambo mengine mengi ambayo yametokana na ukuaji wa teknolojia. Pia kumekuwa na mabadiliko ya nishati inayotumia katika uendeshaji magari ambapo sasa hivi kuna magari yanayotumia umeme na sio mafuta kama ilivyozoeleka.

Treni ni chombo cha usafiri kinachotumika kusafirisha watu na mizigo kwa wingi, chombo hichi cha usafiri hutumia njia maalum ya reli inayoiwezesha kupita maeneo mbalimbali bila kuingiliana na vyombo vingine vya usafiri kama magari. Treni ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1804 nchini Uingereza na ilikuwa inatumia nishati ya mvuke kuendeshea mitambo (steam engine). Kutokana na ukuaji wa teknolojia treni za sasa hivi zinatumia mafuta, umeme na kuteleza kwa sumaku (magnetic levitation). Treni za umeme zinasifika kwa kuwa na spidi kubwa ya kusafiri inayofika hadi kilomita 460 kwa lisaa (460km/hr).

Ndege ni chombo cha usafiri kinachotumika na watu wachache zaidi duniani, na hii ni kutokana na gharama za usafiri kuwa kubwa. Mamlaka ya usafiri wa anga Duniani ICAO ilisema kuwa idadi ya watu wanaosafiri kwa ndege kwa mwaka ni chini ya 6%. Ndege ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1903 na Orville na Wilbur Wright (The Wright Brothers). Ndege hii ilikuwa na uwezo wa kuelea tu angani bila kuwa na nishati yoyote ya kuisukuma. Teknolojia ya sasa ya ndege imefika mbali sana kwani kuna ndege zenye spidi kubwa kushinda sauti na ndege hizi hufahamika kama Super sonic jets. Mfano mzuri wa ndege hizi ni Concorde, Boom pamoja na ndege za kivita za nchi mbalimbali.

Katika vyombo vyote vya usafiri, Meli ndo chombo cha usafiri cha zamani kuliko vyote duniani. Chombo hichi kilianza kutumika miaka ya 7500BC. Meli za zamani zilikuwa ni za mbao na zilihitaji watu kupiga makasia ili iweze kusafiri. Meli za kisasa ni kubwa zaidi ya zile za zamani, zinatumia injini kusukuma mapropela ya kuliendeshea na mafuta kama nishati. Pia meli hizi zimetengenezwa kwa chuma. Kwa miaka ya zamani meli zilitumika sana kusafirisha abiria wanaotokea mbali ila kwa sasa kazi kubwa ya meli ni kusafirisha mizigo, na hii ni kutokana na kuwepo kwa usafiri wa ndege ambao ni wa haraka zaidi kusafiri.

No Comment! Be the first one.