Utiririshaji wa video ni kitendo cha kuangalia video moja kwa moja mtandaoni kwa wakati halisi au kuwasiliana na mtu kwa njia ya video ya wakati halisi. Mpaka sasa kuna majukwaa mengi yanayotoa huduma hizi lakini Teknokona leo tunakuletea orodha ya majukwaa maarufu ya utiririshaji wa video mtandaoni.
Zoom: Hili ni jukwaa linalotumika na takriban watu milioni 300 kwa siku. Jukwaa hili hutumika kuendeshea mikutano mtandaoni, Vikao vya mtandaoni, Kufundishia watu mtandaoni pamoja na matumizi mengine ya utiririshaji wa video mtandaoni. Jukwaa hili pia linawezesha watumiaji kurekodi video zao kwaajili ya matumizi ya baadae.
Microsoft Teams: Ni jukwaa la utiririshaji wa video mtandaoni linalomilikiwa na kampuni ya Microsoft. Jukwaa hili lina uwezo wa kupokea watumiaji 300 kwa wakati mmoja pia lina ulinzi wa kutosha unaotumika kuzuia wadukuzi wasiingilie utiririshaji huo wa video. Microsoft Teams ina watumiaji takriban milioni 250 kwa siku, na wastani wa watumiaji milioni 80 kwa mwezi.
Skype for Business: Skype ni moja kati ya majukwaa ya kwanza ya utiririshaji wa video kwa wakati mtandaoni. Jukwaa hili lilianza kutumika kwenye kompyuta na baadae kuwa na App ambayo inafanya kazi kwenye simu janja. Jukwaa hili lina uwezo wa kumudu takriban watumiaji 250 kwa wakati mmoja na hutumika kufanya vikao vya kiofisi mtandaoni pamoja na mambo mengine.
Google Meet: Hili ni jukwaa la Google maalum kwaajili ya kutiririsha video kwa wakati mtandaoni. Jukwaa hili linatumika sana na watu mbalimbali kwani ukiwa tu na account ya Google utaweza kuitumia huduma hii. Jukwaa hili linaweza kutumika na watu 500 kwa wakati mmoja na lina watumiaji takriban milioni 100 kwa siku.
No Comment! Be the first one.