Mwaka 2023 umeshaanza, heri ya Mwaka Mpya kutoka timu nzima ya Kona ya Teknolojia / Teknokona. Leo tunakuletea orodha ya makala 10 zilizosomwa zaidi mwaka 2022. Makala kutoka masuala ya maujanja ndizo zinazoongoza kwa kusomwa zaidi.

Hizi ndio makala 10 zilizosomwa zaidi kwa mwaka 2022 kupitia blogu yako namba moja ya habari na maujanja ya kiteknolojia.
Namba 1: Emoji na Maana Zake! #Emoji
Makala namba moja ni makala inayozielezea emoji zote maarufu zinazopatikana katika vifaa vyetu vya elektroniki katika upande wa mitandao ya kijamii. Makala hii inakupa maana ya emoji zote maarufu.
Soma makala nzima hapa – > Emoji na Maana Zake! #Emoji
Namba 2: Njia rahisi ya kupata PUK ya kadi yako ya simu
Makala ya pili ni inayoonesha njia ya kupata namba ya PUK kwa watumiaji wa simu, hasa wale wanaotumia mtandao wa Tigo. Kutokana na changamoto hii kuwa maarufu, tunategemea kuandika makala mpya ya kuwasaidia watumiaji wa mitandao yote.
Soma makala nzima hapa -> Njia rahisi ya kupata PUK ya kadi yako ya simu
Namba 3: Orodha ya Ndege Kubwa kuliko Zote Duniani
Moja ya ndege ambayo ilikuwa kwenye orodha hii imekuwa mhanga wa vita kati ya Urusi na Ukraine, hii ni baada ya ndege ya Antonov An-225, iliyokuwa inashikilia namba moja katika nafasi ya kuwa ndege kubwa kuliko zote duniani, kulipuliwa na makombora ya Urusi. Ndege hiyo iliharibika ikiwa eneo la matengenezo katika moja ya viwanja vya ndege nchini Ukraine.
Fahamu kuhusu ndege hiyo na zingine nyingi kwa kusoma makala nzima hapa -> Ndege Kubwa kuliko zote Duniani
Namba 4: Jinsi Ya Kufuta Akaunti Ya Facebook Moja Kwa Moja!
Moja ya makala tuliyoiandika miaka mingi zaidi, takribani miaka 7 iliyopita…. inaonekana watu wengi wanataka kufuta akaunti za Facebook kwa sababu moja au nyingine. Tutahakikisha makala hii inapitiwa na kutolewa toleo jipya ili kuwasaidia wale wenye uhitaji.
Isome hapa ->Jinsi Ya Kufuta Akaunti Ya Facebook Moja Kwa Moja!
Namba 5: FAHAMU: Jinsi Ya Kuandika Barua Pepe (E-mail) Kama Mtaalam!
Mawasiliano ya kikazi siku hizi kwa asilimia kubwa yanahusisha utumiaji wa barua pepe. Kupitia makala hii utapata dondoo zinazoweza kukusaidia katika uandishi wa barua pepe. Nayo ni ya miaka 7 nyuma, hivyo tutaifanyia kazi na kuwaletea toleo jipya.
Isome hapa -> FAHAMU: Jinsi Ya Kuandika Barua Pepe (E-mail) Kama Mtaalam!
Namba 6: Fahamu Kuhusu Kipimo cha HIV Kinachotumia Simu Janja
Namba sita inachukuliwa na habari kuhusu teknolojia ambayo ingewezesha upimaji wa maambukizi ya magonjwa kama vile VVU na mengineyo. Kifaa hicho kilitambulishwa mwaka 2015, ila inaonekana ni teknolojia iliyoishia kwenye majaribio zaidi. Hakuna habari za uingizwaji wake sokoni hadi leo.
Isome hapa -> Fahamu Kuhusu Kipimo cha HIV Kinachotumia Simu Janja
Namba 7: Namna ya kuboresha Betri la Simu lisiishe Chaji Haraka.
Namba 7 inachukuliwa na makala inayolenga kukupa uelewa na dondoo muhimu katika masuala yote yanayohusisha kuchati kwa simu yako, na jinsi ya kufanya ili kuhakikisha unadumisha ubora wa kuhifadhi chaji wa betri lako.
Isome hapa -> Namna ya kuboresha Betri la Simu lisiishe Chaji Haraka. #Maujanja
Namba 8: Njia 3 Za Ku ‘Reset’ Simu Ya Android!
Iwe kwa sababu ya kuboresha ufanisi wa simu yako au kama unahitaji kuiuza simu yako, makala hii inakupa dondoo ya jinsi kuweza kuifuta na kuanza upya.
Isome hapa -> Njia 3 Za Ku ‘Reset’ Simu Ya Android!
Namba 9: Programu 6 Muhimu za Kuwa Nazo kwenye Kompyuta yako ya #Windows10
Kwa watumiaji wa Windows 10 na ata wale wa Windows 11, makala hii inawapa ushauri kuhusu programu muhimu za kutozikosa kwenye kompyuta yako.
Fahamu zaidi -> Programu 6 Muhimu za Kuwa Nazo kwenye Kompyuta yako ya #Windows10
Namba 10: Kujua IMEI Ya Simu Iliyopotea Au Kuibiwa! #Maujanja #Android #iPhone
IMEI ni namba muhimu ya utambulisho wa kipekee wa vifaa vya elektroniki. Kwenye simu kwa kupitia IMEI unaweza kuandikisha kesi ya ufuatiliaji wa simu iliyopotea. Ila inaweza ikatokea ukawa umeibiwa kabla ya kuweka rekodi ya namba hii, makala hii inakupa njia za kupata IMEI namba ya simu yako ata kama haipo mikononi mwako kwa muda huo.
Fahamu zaidi -> Kujua IMEI Ya Simu Iliyopotea Au Kuibiwa! #Maujanja #Android #iPhone
Vipi kuhusu YouTube? Bofya hapa
Video 4 Zilizotazamwa Zaidi kwenye Akaunti yetu ya YouTube 2022. #KonaYaTeknolojia
Je ulikuwa umeshasoma makala ngapi katika orodha hii?
Kumbuka kuangana nasi kwenye mitandao ya kijamii na utuambia ni nini ungependa tusikose kukiandika kwa mwaka huu. Heri ya mwaka mpya.
No Comment! Be the first one.