Makanisa ya Kiprotestanti maeneo ya kati nchini Ujerumani yatakuwa yakiwapa waumini fursa ya kuingia katika mtandao, kwa kuwawekea huduma ya wi-fi bila malipo.
Huduma hiyo itapatikana katika maeneo ambayo, kwa kufuata ‘hostpots’ ambalo ni jina la vitovu vya huduma, yamepewa jina “Godspots”.
Huduma hiyo ya Wi-fi itawekwa katika makanisa 220 katika majimbo ya Berlin na Brandenberg.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha RBB, mpango huo baadaye utatekelezwa katika makanisa 3,000. Makanisa ya kwanza kupata huduma hiyo yatakuwa kanisa kuu la “French Cathedral” eneo la “Gendarmenmarkt” na kanisa la “Kaiser Wilhelm Memorial Church”.
Watu wataweza kutumia huduma hiyo kutoka ndani na nje ya kanisa. Wanaotumia huduma hiyo watakutana na ukurasa wa tovuti yenye maelezo kuhusu kanisa lenyewe, jamii ya eneo hilo na maelezo ya kidini. Lakini pia wataweza kutembelea mitandao mingine pamoja na kudownload chochote.
One Comment
Comments are closed.