Ili simu iendelee kutumika kwa mda mrefu inahitaji iwe na chaji ya kutosha, bila kuwa na chaji/charge ya kutosha simu itazima na utalazimika kuichaji mara kwa mara, kuna vitu vya msingi vya kuangalia pindi unapochaji simu yako ili kuifanya ikae na chaji (charge) kwa mda mrefu na kutunza betri (battery) ya simu ili iweze kudumu zaidi.
Tumeona simu nyingi zinakufa betri (battery) kwa mda mfupi toka simu inunuliwe, hii inatokana na makosa ambayo tunafanya wakati wa kuchaji simu zetu, na mara nyingi watumiaji hawajali namna bora ya kuchaji vifaa vyao hii ni kutokana na kutopata maelekezo mazuri kutoka kwa watengenezaji wa simu au wauzaji wa simu.
JINSI YA KUCHAJI SIMU YAKO VIZURI.
- TUMIA CHAJI RASMI ( USE OFFICIAL CHARGER)
Kutumia chaji ambayo siyo rasmi au siyo maalumu kwa kifaa husika ni moja ya kosa ambalo hufanywa na watumiaji wengi wa simu, wengi huwa tunaangalia tu kama chaji inaingiliana na simu husika, kila simu huja na chaji yake kwenye box la simu ingali ikiwa mpya, tofauti hapo inakupasa ununue chaji ya kifaa husika kutoka kwa wauzaji rasmi au duka la kuuza vifaa hivyo, sababu kila simu ina aina yake tofauti ya kupokea umeme.
2. USISUBIRI MPAKA SIMU IISHE CHAJI NDIPO UICHAJI (DON’T ALWAYS LET IT FINISH CHARGING)
Inashauriwa kuchaji simu yako pindi ikifikia 20% ya uwezo wa betri na mara nyingi simu hutuma ujumbe au kuonyesha alama kwenye betri kuashiria betri inahitaji kuchajiwa, ukiona hizo dalili/alama unaweza kuichaji simu yako. wataalamu wanasema simu hupeleka chaji kwa haraka kuanzia 20% – 80% baada ya hapo inakuwa inapeleka taratibu mpaka kufikia 100% ambapo huacha kupeleka chaji.
3. ONDOA CHAJA KWENYE SOKETI PINDI SIMU INAPOJAA (REMOVE THE CHARGER FROM THE SOCKET IMMEDIATELY)
Simu za kisasa zina uwezo wa kuacha kupeleka chaji (cease charging) pindi simu ikifikisha 100% lakini hiyo haileti uhalali kuwa chaja itaacha kufanya kazi, tunashauriwa kuiondoa simu kwenye chaji pindi tu inapojaa.
4. USIWEKE SIMU SEHEMU YENYE JOTO WAKATI WA KUCHAJI
Halijoto (Temperature) ni kitu cha muhimu sana katika kuboresha maisha ya betri ya simu yako, na hii huenda ikawa ni sababu kubwa ambayo hufanya betri za simu zetu kuharibika kwa haraka, halijoto (Temperature) ikiwa kubwa hasa wakati wa kuchaji husababisha betri kuharibika/kufa mapema kuliko simu ambayo imewekwa kwenye halijoto la chini.
5. USITUMIE SIMU WAKATI WA KUCHAJI
Hili ni kosa kubwa ambalo wengi tunalifanya bila kujua, simu haiwezi kufanya kazi mara mbili kwa usahihi, simu iingeze chaji na kutumia chaji kwa wakati mmoja hii inaua cells za kwenye betri maana betri hutumia nguvu isivyo kawaida, kingine inaharibu mzunguko wa kuchaji simu (charging cycles), kama simu ilitakiwa ijae ndani ya dakika 30 basi itatumia dakika 50 au zaidi na hii hufanya betri kupata joto na hupelekea kuharibu kabisa betri ya simu.
USHAURI
- Kuchaji simu yako na ukaishia 80% – 90% ni bora zaidi kwa afya ya betri kuliko kufikisha 100%.
- Epuka simu yako kuishiwa chaji kabisa yaani 0% ya betri, na kulaza simu yako kwenye chaji mara kwa mara.
- Joto husababisha kuharibu betri, jitahidi kuweka simu sehemu isiyo na joto kali, pia usifunike simu wakati wa kuchaji.
- Usitumie simu wakati wa kuchaji, hasa hasa usitumie kwa kazi nzito kama kucheza games, kuangalia video mtandaoni (streaming).
No Comment! Be the first one.