WhatsApp ni moja kati ya mitandao wa kijamii ambayo ni maarufu sana na ina watumiaji wengi, mara kwa mara mtandao huo umekua ukifanya maboresho kadha wa kadha.
Maboresho haya katika mtandao huwa yanasiaidia katika kuhakikisha kuwa watumiaji wa WhatsApp wanapata kile kilichobora wakiwa wanatumia huduma hiyo.
Kwa sasa kuna sasisho ambalo limefanyika na linakita sana katika makundi (Groups) ndani ya mtandao huo.
Kwa haraka haraka ni kwamba katika makundi hayo wale wakuu/wasimamizi/waandaaji (admin) watakua na uwezo mkubwa wa udhibiti juu ya nani ajiunge na kundi husika.
CHAGUA NANI AINGIE NDANI YA KUNDI
Kwa wale ma’admin kwa sasa watakua na uwezo wa kuwakubalia watu au kukataa kabisa kujiunga na kundi husika.
Kingine kizuri kuhusiana na kipengele hiki ni kwamba rekodi ya watu waliokubaliwa au kukataliwa zamani zitabakia kwa ajili ya Admin kuziona ili kufanya maamuzi sahihi.
KIPENGELE CHA ‘GROUPS IN COMMON’
Ni wazi katika makundi kuna mengi yamefanywa na WhatsApp nadhani unakumbuka hata mwaka jana kipengele cha Community kilitambulishwa rasmi. Soma Zaidi >>HAPA<<
Katika kipengele cha Groups In Common hapa ni kwamba WhatsApp wana kipengele mahususi kabisa katika kukutaafu kwamba ni makundi gani ambayo upo pamoja na mtu fulani.
Hii itakata kabisa ile adha ya kujaribu kukumbuka kuwa nani uko nae kwenye kundi moja bila ya kupoteza muda na kwa urahisi kabisa
Vipengele hivi ni muhimu sana katika mtandao wa WhatsApp maana vina msaada mkubwa na hata ukiachana na hayo kuna maboresho mengine madogomadogo yamefanyika.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je umeshaanza kutumia vipengele hivi? Kama bado hakikisha kuwa una toleo jipya kabisa la WhatsApp.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.