Umewahi kufikiri unaweza kuweka mwongozo wa matamshi ya jina lako Facebook? Au siku ukiachana na mwenzi wako, utabadili vipi ‘notification’ yako ya ‘In-Relationship’ au ‘married’ bila ya marafiki zako zaidi ya 2000 kufahamu? Kuweka maandishi ya rangi zinazovutia katika picha unazozituma Facebook?
Huna haja ya kuwa na wasi wasi tena, Facebook wanashughulika kila siku kutimiza mahitaji ya mabilioni ya watumiaji na kuongeza huduma tofauti kila siku.
Mambo haya MATANO mapya yameongezwa na Facebook kukidhi haja zako.
1. Ongeza Matamshi ya Jina Lako
Watumiaji wa Facebook duniani kote huzungumza zaidi ya lugha 80 tofauti. Kuna Wazungu, Waarabu, Wachina, Wafaransa, Watanzania na mataifa mengine mengi yanayozungumza lugha tofauti. Watu wote hawa, huweza kutamka jina lako tofauti na wewe unavyotaka.
Katika Facebook, unaweza kuwaongoza marafiki namna jina lako linavyotamkwa.

Kuongeza matamshi, nenda kipengele imeandikwa ‘About’ katika profile yako na kisha bonyeza ‘details about You (Pia ‘more about you’ kama unatumia simu’)’ kisha chagua, ‘name pronunciation’. Facebook watapendekeza namna jina lako linavyotamkwa, na utasikiliza kuchagua. Kama hakuna, utaandika matamshi yako mwenyewe ya kifonetiki ya jinsi unavyotaka litamkwe.
2. NenoSiri (Password) la muda mfupi.
Wakati mweingine ni hatari kuingia katika ukurasa wako wa Facebook kwa kutumia Kompyuta za Umma, au kompyuta ya mtu mwingine. Kunaweza kuwa na program maalum za kuibia nenosiri lako, au kusahau kutoka (Log out), na mtu mwingine akija kutumia akakuta akaunti yako iko hewani, akasoma mambo yako, kuiba data zako na hata kutumia akaunti yako kupost vitu usivyotegemea.
Kuepuka hili, Facebook wanakuwezesha kuomba nenosiri la muda mfupi, kwa kutuma neno ‘OTP’ kwenda namba 32665.

Watakutumia nenosiri la muda mfupi utakaloweza kutumia ndani ya dakika 20 na halitaweza kutumika tena.
3. Chagua ‘Notification’ Unazotaka kuona
Umewahi kucahngia kwenye posti yeyote Facebook na baada ya apo unakua ukipokea ujumbe unasema “James Jackson and 5 Others commented on a post”. Huwa zinakera wakati mwingine.

Unaweza kuzuia ujumbe kama huu kwa kubonyeza alama ndogo ya ulimwengu karibu na kitufe cha message, kisha alama ya X iliyo karibu na posti unayotaka kuzuia ujumbe wa aina hiyo.
4. Fanya picha unazoposti zivutie zaidi
Uwezo mpya maarufu japo unajulikana na watu wachache unakuwezesha kupamba kabla ya kutuma picha zako kwa kuingiza maneno, stika mbalimbali kama miwani, kofia n.k. Kufanya ivi, utavutia marafiki wako na kupata Likes nyingi kwa washkaji bomba zaidi.
Huduma hii inapatikana katika simu za iPhone pekee, lakini punde na simu za Android zitawezeshwa. Kutumia, chagua picha unayotaka kutuma, kisha bonyeza alama ya magic chini ya picha hiyo, kisha chagua stika mbalimbali na maneno ya kuongeza kwenye picha yako.

Waulize washkaji, apo vipi?
5. Zuia watu kuona ishara ya mahusiano yako Facebook.
Wakati wa kutangaza kwenye Facebook kuwa umepata mchumba, umeoa au umeolewa huwa ni furaha na huvutia sana. Watu hu-like picha zako, kukupa pongezi nyingi na vitu vingi vizuri. Vipi siku ukitengana nae? Utabadilisha kuwatangazia marafiki zaidi ya 2000 kuwa ‘divorced’ au ‘single’. Hakuna haja tena ya kuhofia kutangaza kuachana na mwenzi wako kwa marafiki. Sasa unaweza ukabadilisha na kuweka mwisho wa Uhusiano wako bila mtu yeyote kuona.

Nenda katika profile yako, bonyeza about, kisha nenda katika ‘family and relationship’ upande wa kushoto, chini ya ‘relationship’ utaona kitufe cha udhurungi kilichoandikwa ‘friends’ au ‘public’. Badilisha na kisha weka ‘Only me’.
Sasa unaweza kubadili status ya Uhusiano wako mara nyingi uwezavyo.
No Comment! Be the first one.