Sio kitu cha ajabu kabisa kusikia kampuni fulani inafanyia kazi jambo fulani ambalo linatokana na maoni ya watu/wateja wa bidhaa fulani. Vivyo hivyo Apple wapo katika maboresho ya vitu mbalimbali ambavyo vina mashiko katika ulimwengu wa teknolojia.
Unapofikiria kuboresha kitu fulani ni jambo ambalo wakati mwingine linahitaji mawazo na fikra pevu kuweza kufanya kitu kilicho bora zaidi kuliko kile ambacho kimepita huko nyuma. Ndio, Apple ambao hivi sasa wana iOS 13 inatazamiwa kuja na maboresho kadhaa kama vile kipengele cha muonekano wa giza ambao ni mpana zaidi, pamoja na mengineyo kadhalika.
Tofauti na maboresho/vitu ambavyo Apple wanaviboresha vipo vingine ambavyo vinatumiwa na watu wanaotumia bidhaa zilizo chini ya kampuni hiyo katika mzunguko wa maisha ya teknolojia mathalani:-
- kuunganisha ‘Find my iPhone‘ na ‘Find my Friends‘. Hivi sasa hizo ni programu tumishi mbili tofauti ambazo zinatumika kwenye iOS na macOS lakini imeelezwa kuwa Apple wapo kwenye matengezo ya kuzifanya programu hizo zipatikane sehemu moja na kufahamika kama “Green Torch“. Programu tumishi zitakuwa zikifanya kazi zake zilezile za awali tofauti yake itakuwa zitapatikana ndani ya mwamvuli mmoja iwe kwa iOS au macOS.
Find my iPhone: Moja ya Mambo ambayo Apple wanaboresha ni programu ya kutafuta iPhone/rafiki iliyopotea. - uwezo wa kuitafuta simu iliyopotea bila ya usaidizi wa intaneti. Tulio wengi tunafahamu kuwa inawezekana kuipata simu iliyopotea iwapo ikiunganisha kwenye intaneti, sasa Apple kupitia kipengele cha ‘Find Network‘ wanataka kuwezesha kuipata simu ikiwa haijaunganishwa kwenye intaneti,
- kifaa cha kutafuta kitu. Tumezoa kutumia programu fulani kutafuta vifaa vyetu vya kidijiti lakini sasa Apple wanatengeeza kifaa ambacho mtu ataweza kukigusisha na kitu kingine ambapo kitakuwa kimeunganishwa na akaunti ya iCloud ya mlengwa, mhusika ataweza kupata taarifa fupi iwapo ametoka nje ya umbali ambao haustahili. Vilevile, kifaa hicho kitaweza kutunza taarifa fulani ambazo zitaweza kuonekana kwenye bidhaa nyingine za Apple na hata kuweza kusambaza kwa marafiki/ndugu mahali kilipo kifaa hicho,
- kupata taarifa fupi iwapo ndugu/rafiki anapoondoka au anapofika mahali fulani. Katika maboresho mtu ataweza kujua pindi tu ndugu/rafiki yake anapotoka sehemu moja kwenda nyingine.