Katika ulimwengu wa kisasa, simu janja ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku. Kutoka kwa sababu za mawasiliano, urambazaji, hadi burudani, vifaa hivi tunavitumia mara kwa mara. Moja ya changamoto kubwa katika matumizi ya simu janja ni kudumisha ubora wa betri ya simu yako.
Inaweza ikawa umewahi kusikia vidokezo vingi vya kufanya ili betri yako idumu, lakini ni muhimu pia kujua mambo ambayo hupaswi kufanya. Hapa kuna orodha ya mambo unayopaswa kuepuka ili betri ya simu yako idumu kwa muda mrefu.
1. Usitumie Chaja Feki au Zisizo Rasmi
Kutumia chaja zisizo rasmi au feki ni moja ya makosa makubwa ambayo unaweza kufanya. Chaja hizi mara nyingi hazina viwango sawa vya usalama kama zile rasmi na zinaweza kuharibu betri ya simu yako. Hakikisha unatumia chaja iliyotolewa na mtengenezaji wa simu yako au iliyothibitishwa.
2. Usiachie Simu Yako Ipate Joto Sana.
Mionzi ya joto inaweza kuharibu betri ya simu yako haraka. Ikiwa unatumia simu yako kwa kazi nzito kama magemu au matumizi ya muda mrefu ya GPS, hakikisha unaiweka katika sehemu yenye hewa ya kutosha. Pia, usiiache simu yako kwenye gari lililo kwenye jua kali au karibu na vifaa vinavyotoa joto kali.
3. Usisahau Kuzima Programu Zinazotumia Nishati Nyingi
Programu zinazoendelea kufanya kazi hata kama huzitumii zinaweza kutumia nishati nyingi bure. Hakikisha unazifunga programu ambazo hutumii mara kwa mara. Unaweza pia kutumia kipengele cha ‘battery saver’ kilichopo kwenye simu yako ili kusaidia kuokoa nishati.
4. Usitumie Betri Mpaka Ifikie Asilimia 0%
Kutumia simu yako hadi betri yako ikifika asilimia 0% inaweza kupunguza ubora wa betri ya simu yako. Ni bora kuanza kuchaji betri yako ikiwa imefika asilimia 30% hadi 20%. Hii inasaidia kuepuka mizunguko ya kuchaji kupita kiasi, ambayo inaweza kuharibu betri yako kwa muda.
5. Usitumie Simu Yako Wakati Inachajiwa
Kutumia simu yako wakati inapochajiwa huongeza joto na inaweza kuathiri betri yako. Hii ni tabia inayoweza kuharibu betri haraka. Ni bora kuiacha simu yako ikichaji bila kuitumia ili kuepuka uharibifu wa betri.
6. Usisahau Kufanya Sasisho(updates) za Programu
Watengenezaji wa programu mara nyingi hutoa masasisho ambayo yanaweza kuboresha matumizi ya nishati ya simu yako. Usipuuze ujumbe wa kufanya sasisho(updates) za programu zako kwani zinaweza kusaidia kupunguza matumizi ya nishati na kuongeza ufanisi wa betri yako.
7. Usitumie Mwanga wa Skini wa Kiwango cha Juu
Mwanga wa juu wa skrini inatumia nishati nyingi. Badala yake, tumia kipengele cha kurekebisha mwanga kiotomatiki au punguza mwanga wa skrini yako mwenyewe. Hii itasaidia kupunguza matumizi ya nishati na kuongeza muda wa betri yako.
Hitimisho
Kuepuka mambo haya rahisi kunaweza kufanya tofauti kubwa katika utendaji na maisha ya betri yako ya simu. Jinsi utaratibu huu ili kudumisha ubora wa betri ya simu yako na utumie simu yako bila wasiwasi wa betri kuisha haraka.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.