Ni rahisi sana kuweza kutokuwa muangalifu katika kushusha mafaili mtandaoni kwa sababu zoezi zima linafanyika baada ya wewe ku’click’ maeneo kadhaa tuu
Kuwa makini sana huwezi jua nyayo unazofuata katika kuhakikisha unashusha mafaili yako zitakufikisha wapi
Tukiepuka Makosa Haya Basi Tutaweza Kushusha Mafaili Yetu Kwa Usalama Kabisa
1. kutoShusha Mafaili Katika Vyanzo Vinavyofahamika
Kuna mamilioni ya Apps na mafaili mengine mengi katika mtandao. Kuna muda mwingine unaweza ukashusha faili ambalo likaleta matatizo katika kifaa chako. Hii haijalishi kama unatumia kifaa cha Windows, Mac, Android au hata iOs
Ili kujiweka salama inakubidi uzuie App na programu mbalimbali ambazo zinatoka katika vyanzo ambavyo havijulikana/tambuliku kutoweza kuingia katika kifaa chako
Kwa Android nenda Settings >> Application Settings >> Zima Uknown sources
Kwa Windows 10 nenda Settings >> Update & Security >> For developers >> na kisha zima ‘Sideload Apps’ na ukitaka kushusha kitu tumia App ya ‘Windows Store’
Kwa Mac ingia katika System preference >> Security & Privacy >> click alama ya kufuli na kisha ingiza neno siri (password) baada ya hapo hakikisha unachagua ‘Mac store and identified developers only’ au ili kujiweka salama zaidi chagua ‘Mac Store Only’
Kwa iOs kama simu yako hujai ‘jailbreak’ upo salama kwani hakuna njia nyingine ambayo unayoweza kutumia katika kushusha App ukiachana na App store tuu
2. Kutofanya Uchunguzi Kuhusiana Na App Unayotaka Kuishusha
Kabla hujashusha App yeyote au hata programu kuwa na katabia kakufanya uchunguzi kwanza katika mtandao. Unaweza ukaingia Google na kisha ukaandika jina la programu hiyo na mwishoni pale ukamalizia na neno ‘Scam’, ‘virus’,’safe’ na kisha angalia majibu gani yatakuja
Hata siku moja usiamini Reviews zile ambazo zinakuwa katika App yenyewe kwa ndani, kumbuka ile inaweza ikawa ni lugha ya kibiashara zaidi
3. Usipendelee Kushusha Mafaili Ambayo Yapo ‘Cracked’ Au Ya Wizi
Ukiona kuna namna unaweza ukajipatia programu ambayo inauzwa bure katika mtandao usiikimbilie programu hiyo kwani kuna hati hati kubwa inaweza ikaleta madhara katika kifaa chako. Kumbuka software ambazo zipo ‘cracked’ nyingi zinakuwa zimebadilishwa mambo kadhaa ukifananisha na zile zinazouzwa
Hii inamaanisha kuwa huwa haziangaliwi na watu halali wakati wa kuzipandisha katika mtandao hivyo basi inamaanisha kuwa hata wale ‘hackers’ wana uwezo wa kupandikiza kitu chochote katika programu hizo ambacho kikaleta madhara kwa kifaa chako
4. Usishushe Mafaili Kabla Huja’Scan’ Virus
Ukiachana na vingi vizuri ambavyo intaneti inakuja navyo pia kuna mabaya ambayo yanaweza yakapatikana humo. Ni vibaya sana kuzurura mtandaoni kama hauna Anti virus ya kukulinda.
Na lingine la muhimu ni kwamba inakubidi mtu uwe unatumia Anti virus kuweza kuscan programu Fulani kabla ya kuzishusha katika kifaa chako.
Windows 10 ina ‘Windows Defender’ moja kwa moja ambayo unaweza ukaitumia kwa matoleo mengine inakubidi uchukue ulinzi kutoka Kaspersky (Anti Virus ya Kaspersky)