Je betri za simu huwa zinalipuka? Ndio, huwa inatokea na huwa inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, leo fahamu ni nini hasa cha kufanya kuepuka jambo ili kutokea. Kumbuka kusambaza makala hii kwa ndugu na marafiki ili nao waweze kuwa salama siku zote pale wanapofanya maamuzi ya kununua simu au pale wanapotumia simu zao.
Kitu cha kukumbuka ni kwamba kwa kiasi kikubwa betri za simu siku hizi zinatengenezwa chini ya uangalizi mkubwa na wa kiteknolojia ya juu. Mara nyingi pale zinapokuwa na tatizo mara nyingi huwa kwa sababu ya kutumia betri au chaja zilizotengenezwa chini ya viwango na makampuni yasiyo rasmi, na ata pale inapokuwa imetokea nje ya sababu hii basi itakuwa imesababishwa na sababu zingine zisizo za kikawaida.
>Hakikisha unanunua simu au betri zenye ubora/kiwango cha juu.
Hakikisha unanunua simu iliyo kwenye kiwango na ubora salama. Je ni simu kutoka kwenye kampuni inayoaminika? Pia angalia kama ni ‘original’ kwani kuna makampuni mengi kutoka Uchina huwa yanaiga umbo na vitu vingine mbalimbali vya simu maarufu duniani na kuzitengeneza zikiwa chini ya viwango. Simu zilizochini ya viwango kutoka makampuni ya simu yasiyoeleweka ni hatari kwako. Na rudia tena, NI HATARI SANA KWAKO!
Pia angalia kama betri katika simu yako imeandikwa taarifa muhimu zinazofanana na chaja iliyoambatanishwa nayo. Usikubali kununua betri lisilokuwa na maandishi yeyote yale, mfano ya taarifa za volti (voltage) inayotumia ambayo inatakiwa kuwa sawa na iliyo kwenye chaja yake.
>Usiache simu yako katika mazingira ya joto sana!
Upo jikoni? weka simu yako mbali na joto kali, pia ata kama ni nje usiiache kwenye miale ya jua kali kwa muda mrefu. Joto hili linaweza sababisha mlipuko wa betri husika, na ata kama haitalipuka muda huo basi ujue unaharibu ubora wake.
>Ukiwa unaichaji!
Hakikisha ipo mbali na eneo lenye joto kali.
Pia kama inakubidi upokee au upige simu basi ichomoe kutoka kwenye chaji.
>Usiku!
Hakikisha unaweka simu yako umbali kidogo kutoka unapolala, mfano weka kwenye stuli au meza iliyo pembeni ya kitanda chako. Usilale na simu kitandani, kwa sababu hii itamaanisha itakuwa karibu na eneo la kichwa chako, hii ni hatari sana kwani kama kutakuwa na kitu ambacho hakiko sawa katika simu hiyo na kuifanya ilipuke basi utakuwa kwenye hatari sana. Wengine huwa wanachaji simu usiku kucha huku wakiiweka simu hiyo kitandani pamoja nao, hili ni jambo la hatari.
>Uwe unaipa muda simu kupoa baada ya matumizi mazito na ikapata joto kali!
Ndio mara nyingine utakuta ni wewe ndiye umeitumia simu muda mrefu bila kuipumzisha na ata simu hiyo ikaanza kupata joto kali, ikitokea simu yako imeshika joto sana iweke sehemu ipate kupoa na ndiyo uitumie tena.
Je uchaji simu yako ikiwa na kiwango gani kuzidi kuifanya betri iwe kwenye ubora mzuri?
Watafiti wanakushauri kama betri ya simu yako ni ya ‘Li-ion’ hakikisha mara nyingi inakuwa na chaji zaidi ya asilimia 50, mara nyingi betri za simu hizi zinakuwa zinaharibika kama zinakuwa zinakuwa chaji ndogo mara kwa mara.
Je umejifunza kipya leo? Tuambie 🙂 Na kumbuka kusambaza makala kwa marafiki!
No Comment! Be the first one.