Kwa miaka ya hivi karibuni soko la simujanja (smartphones) limekua kwa kasi sana. Yameibuka makampuni mengi yanayozalisha hizi simu, kampuni zimefungua matawi mbalimbali duniani na pia kuna wauzaji binafsi wa simujanja.
Kwa Tanzania kuna Kampuni maarufu kama Samsung, Transsion (Tecno, Infinix na itel) Vivo, Xiaomi, Oppo n.k. Haya makampuni yana miliki maduka makubwa kwenye mikoa mbalimbali ndani ya hii nchi. Lengo Likiwa ni kuwarahisishia wateja kuzipata simu zao kwa wakati.
Simujanja huuzwa pamoja na Warranty/dhamana na mara nyingi warranty huwa ni kati ya miezi 12 mpaka 24. Hii Warranty mteja hupatiwa pamoja na risiti yake ya kuthibitisha kwamba hiyo simu ni yake ili ikitokea simu imepata matatizo yaliyosababishwa na simu yenyewe mteja atapata suluhisho la tatizo kutoka kwa wauzaji wa simu husika na siyo matatizo yaliyotokana na uzembe wa mtumiaji kama kudondosha simu, kuiingiza kwenye maji ilihali simu ina tahadhari kuwa ikiingia maji itaharibika.
HAKI YA MTEJA/MNUNUZI NA MUUZAJI WA SIMUJANJA JUU YA WARRANTY
Kama ilivyo kawaida ukinunua simu lazima upate na warranty ambayo itakusaidia katika nyanja zifuatazo:
1. Uhalali wa mali uliyoinunua.
2. Usaidizi endapo simu itapata tatizo.
Warranty inasaidia katika nyanja zifuatazo:
(a) Tatizo katika mfumo/software.
Matatizo mengi katika mifumo/software yanayotokea kwenye simu yanalindwa na warranty, mfano Network ina shida, SIM card/laini haisomi, programu endeshi (Operating system) imeleta shida n.k matatizo ya mfumo ambayo husababishwa na mtumiaji mfano ku-flash simu n.k hayapo kwenye warranty.
(b) Tatizo katika vifaa/Hardware.
Hii lazima uielewe vizuri, warranty katika tatizo la vifaa/hardware huwa inasaidia endapo simu imepata tatizo kama shida ya betri, simu kupata moto isivyo kawaida, simu kuganda na kushindwa kufanya kazi (stacking), simu kujibonyeza yenyewe (blink/Ghost touch).
Kwa upande wa tatizo la vifaa (Hardware Problem) warranty haifanyi kazi katika sehemu zifuatazo
• Kuharibika kwa kioo kutokana na uzembe wa mtumiaji, hili tatizo halipo kwenye warranty, mfano umedondosha simu ikapasuka.
• Simu kupata tatizo sababu ya kuingia maji ndani ya simu pia haipo kwenye warranty.
No Comment! Be the first one.