Uchina imeanza kutengeneza manowari yake ya pili spesheli kwa ajili ya ubebaji na uendeshaji wa oparesheni za kivita.
Itatengenezwa kwa kutegemea teknolojia ya nyumbani, taarifa za kutengenezwa manowari hii zimetolewa na wizara ya ulinzi ya taifa hilo kubwa huko mashariki ya mbali. Meli hiyo yenye uzito wa tani 50,000 inatengenezewa katika bandali ya Daliani.
China imekuwa inaongeza nguvu za jeshi lake hasa kipindi hiki ambapo taifa hilo linaloongoza kwa idadi ya watu duniani limekuwa katika migogoro na majirani zake juu ya bahari za mashariki na kusini. Umiliki wa manowari hizi spesheli zenye uwezo wa kusafirisha ndege za kivita na kuruhusu kuruka na kutua kwenye kiwanja chake kunalipa taifa lolote lenye manowari hizi sifa na uwezo wa kuendesha vita mahali popote, hii ikiwa ni mbali na nchi kavu.
Manowari ya kwanza ya kivita kwa ajili ya kubeba ndege na kuendesha oparesheni za kivita ya China inaitwa Liaoning ni meli ya mtumba ambayo ilinunuliwa kutoka kwa Urusi ambako ilitengenezwa miaka 25 iliyopita, meli hii ili kabidhiwa kwa China mnamo mwaka 2012 baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa.
Teknolojia inayotumika kujenga meli hii ni ile iliyopatikana kutokana na mafunzo pamoja na utafiti uliofanyika katika katika Liaoning, hii imefanya kuwe na maboresho pamoja na uwezeshwaji zaidi katika kuifanya meli hiyo mpya inayotengenezwa kuwa bora zaidi ya hii iliyonunuliwa Urusi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia Marekani ndiyo nchi inaongoza kwa kuwa na Meli za aina hii 10 ambazo zinafanya kazi ikifatiwa na India pamoja na Italy ambao wao wanazo mbili mbili zinazofanyakazi, wakati China Hispania Ufaransa Urusi Brazili na Thailand zenyewe zinamiliki meli kama hizo moja moja zinayofanya kazi.
No Comment! Be the first one.