Ni wazi kuwa makampuni ambayo yanajihusisha kabisa na teknolojia huwa kuna muda yanauzwa au hata kununuliwa kwa dau kubwa sana, leo tunakuletea orodha ya makampuni yalionunuliwa kwa dau kubwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita
Mfano mzuri ni mtandao ya kijamii ikiwa inauzwa au kununuliwa mara nyingi inakua inahusisha hela nyingi sana, Leo tutaangazia makampuni 10 ya teknolojia ambayo yamenunuliwa kwa pesa nyingi kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.HII NI SEHEMU YA KWANZA
2022: Microsoft Yainunua Activision Blizzard Kwa Dola Bilioni 68.7 Za Kimarekani.
Mpka mwaka unaisha hili ndio dili kubwa kabisa lililotokea kwenye teknolojia. Kwa kifupi ni kwamba linahusisha kiasi kikubwa cha pesa na pia dili hili limeleta viulizo vingi ambavyo vimepelekea uchunguzi wa kina kufanyika kuhusiana na jambo hili.
Activision Blizzard ni kampuni ambayo inajihusisha na magemu kama vile Call Of Duty na mengine mengi na kwa sasa pengine kampuni hiyo itakua chini ya kampuni ya Microsoft.
2015: Dell Imeinunua EMC Kwa Dola Za Kimarekani Bilioni 67.
Dell sio kampuni ngeni ndani ya masikio na macho yako sio? Pengine umeijua kutokana na umahiri wake katika kutengeneza na kuuza computer sio?
Mwaka 2015 iliingia katika vichwa vingi vya habari baada ya kuinunua kampuni ya EMC ambayo inamiliki VMWare kwa dola za kimarekani bilioni 67 na kujipatia jina kubwa sana kwa muda huo.
2022: Elon Musk Ainunua Twitter Kwa Dola Bilioni 44 Za Kimarekani.
Hii sio ya zamani sana na mauziano haya japokua yalileta ukakasi kwa baadhi ya watu na makampuni ila bado yalifanyika.
Naama kwa sasa bwana Elon ndio anamiliki mtandao huo wa kijamii wa twitter, manunuzi haya yalikamilika kabisa mwishoni mwishoni mwa mwaka 2022.
2015: Avago Iliinunua Broadcom kwa dola za kimarekani bilioni 37.
Kuna muda mwingine majina ya kampuni sio kitu kwa mtumiaji wa mwisho wa huduma au bidhaa. Kwa mfano Avago na Broadcom ni makampuni makubwa sana lakini pengine wengi hawajui majina haya.
Avago wao ni watengenezaji wa chipi huku Broadcom wao ni waandaaji na wasambazaji wazuri wa software zinazohusika sekta miundombinu na hata ‘semiconductor’
Penigne umeshawahi kututumia kifaa chenye vitu kutoka Broadcom au unaweza shangaa hata unasoma hii kupitia kifaa ambacho kina vitu kutoka kampuni ya Broadcom.
2020: AMD Iliinunua Xlinix Kwa Dola Za Kimarekani Bilioni 35.
AMD nae ni mtengenezaji mzuri sana wa Chip na hapa maji yalimfika shingoni na akaamua kumnunua mpinzani wake, Xlinix ndani ya nwaka 2020.
Hii ilikua ni jambo zuri sana kwa AMD kwani baada ya hili walielekeza ushindani wao kwa washindani wao wa siku nyingi, Intel kwa umakini zaidi
Ni wazi kuwa makampuni ambayo yanajihusisha na Teknolojia mara nyingi huwa yanahusika na kutengeneza pesa nyingi sana katika biashara zake na vile vile sekta ya teknolojia ni sekta ambayo inaheshimika sana
Makampuni haya tajwa hapo juu mara nyingi sana watumiji wa huduma wa mwisho wanajuaga kama yanajitengemea ila ukija kuchunguza unagundua kuwa yanamilikiwa na makampuni mengine ambayo ni makubwa zaidi – lakini wakati mwingine hili halina maana sio?
SOMA SEHEMU YA PILI >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani kuna manunuzi mengine ambayo ni makubwa na unahisi nimeyaruka?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.