Mapato ya OpenAI yanaongezeka, OpenAI waliojikita katika utafiti wa teknolojia ya akili ya bandia, wanatarajiwa kuingiza mapato ya zaidi ya dola bilioni 1 mwaka huu. Hii ni ongezeko kubwa kutoka mapato ya dola milioni 28 tu mwaka jana.
Dola bilioni 1 ni zaidi ya Tsh Trilioni 2.
Mapato ya OpenAI yanaendeshwa na ukuaji wa chatbot ya ChatGPT, ambayo imekuwa programu inayokua kwa kasi zaidi katika historia. ChatGPT inaendeshwa na teknolojia ya kikompyuta ya lugha (LLM – Large Language Model) ya OpenAI, ambayo inaweza kuzalisha maandishi, kutafsiri lugha, kuandika aina tofauti za maudhui ya ubunifu, na kujibu maswali yako kwa njia ya kuelimisha.
Mbali na ChatGPT, OpenAI pia inapata mapato kupitia ushirikiano na makampuni na mashirika mengine. Kwa mfano, kampuni imeshirikiana na Microsoft kuunda Azure OpenAI, jukwaa linaloendeshwa kupitia teknolojia ya Cloud na kuwawezesha watengenezaji programu na huduma kuweza kuitumia teknolojia hiyo ya AI katika bidhaa zao.
Ukuaji wa haraka wa OpenAI ni ishara ya ukuaji wa fursa za kibiashara zinazohusisha teknolojia ya AI (akili ya bandia).
Vyanzo vya mapato kwa OpenAI:
- Kutozwa watumiaji wanaotumia huduma yake ya kuchati ya ChatGPT Pro
- Mapato kwa njia ya kuuza leseni ya utumiaji wa teknolojia yake ya ChatGPT kwa makampuni mengine (API)
- Kushirikiana na mashirika mengine kuendeleza na kutekeleza programu za AI, kuna makampuni washirika ambao nao wanachangia fedha zaidi kwa ajili tafiti zinazofanywa na OpenAI
Itachukua muda mrefu shirika hilo kunufaika na ukuaji huu wa mapato, katika mkatapa wa ufadhili wa dola bilioni 13 walioingia na Microsoft mapema mwaka unawapa Microsoft haki ya kupata asilimia 75 ya faida ya katika mapato ya shirika hilo. Haki hii itakwisha pale Microsoft itakaporudisha kiasi hicho cha uwekezaji wake.
Mapato ya OpenAI bado ni madogo ikilinganishwa na makampuni mengine ya teknolojia. Lakini, kampuni hii inakua kwa kasi na inatarajiwa kuzalisha mabilioni ya dola kwa mwaka kama mapato katika miaka ijayo.
vyanzo: Yahoo Finance
No Comment! Be the first one.