Inasemekana kwamba mapigo ya moyo huenda yakachukua nafasi ya mfumo wa alama za vidole katika eneo la usalama. Kwa mujibu wa kampuni ya Bionym Mapigo ya moyo yanaweza kuwa jibu kwa swali la muda mrefu juu ya njia bora zaidi ya kulinda taarifa na vifaa vyetu.
Hadi sasa mifumo mingi ya usalama wa vifaa pamoja na taarifa inatumia zaidi alama za vidole kama ndio njia bora zaidi ya usalama, alama za vidole tayari zinatumika kwaajiri ya kufungua milango, kompyuta na simu lakini njia hii bado imekuwa na mapungufu kadhaa.
Moja ya vikwazo vya njia hii ya alama ya vidole ni kushindwa kumthibitisha mtumiaji ila mpaka pale atakapoweka kidole katika kifaa maalumu, hii ni changamoto hasa pale ambapo uthibitisho unahitajika mara kwa mara.
Kwa upande wake kampuni ya Bionym ambayo inatengeneza kifaa ambacho kitatumika kupima mapigo ya moyo wako ili kufungua vifaa vyako.
Kampuni hii inataka kuleta teknolojia ambayo itamfanya mtu avae kifaa ambacho kitakuwa kinapima mapigo ya moyo kisha kuwasiliana na kifaa chako tuseme simu kwa mfano hivyo kama mapigo ya moyo kiliyoyapima ni yako basi pindi utakapoisogelea tu simu yako basi itafunguka, vivo hivyo pindi utakapo ondoka mbali na kifaa chako basi kitajifunga.
Tofauti na teknolojia ya alama za vidole ambayo inahitaji mtu kusomesha kidole katika sensa maalumu kila wakati anataka kufungua kifaa kitu ambacho sio chepesi kama sheria za usalama zitataka kuthibitisha utambulisho wa mtu mara kwa mara.
Ingawa teknolojia ya usalama kwa kutumia njia hii bado haijaanza kutumika saana, upo ushahidi wa kutosha juu ya kuwa na nafasi kubwa kuja kutumika nyakati zijazo. Imesemekana kwamba kila binadamu anamapigo ya moyo ambayo yanatofautiana na mapigo ya moyo ya mtu mwingine yeyote.
Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus.
Habari hii imeandikwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali mtandaoni.