Katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni na hatimaye rais mpya kuchaguliwa; Facebook imekataa uvumi ya kwamba Facebook iliruhusu watu kueneneza jumbe za uongo kuhusu uchaguzi huo kitendo ambacho matokeo yake si kama ilivyokuwa ikitegemewa.
Uvumi huo umekuja baada ya Rais mteule wa Marekani kuchaguliwa na si yule ambaye aliyekuwa akitegemewa kushinda katika uchaguzi huo kutokana na raia wengi kuonyesha kumkubali kuliko yule aliyeshinda katika uchaguzi huo.
Mmiliki wa Facebook amesema kuwa habari ya kusema kwamba Facebook iliruhusu jumbe na stori mbalimbali za uongo kuhusiana na uchaguzi huo si za kweli na zinatokana na hasira na kutafuta nani wa kumlaumu.

Tetesi zinasema kuwa jumbe hizo ziliweza kuchagiza matokeo hayo ya uchaguzi uliofanyika nchini Marekani hivi karibu lakini kila mtu anamchagua yule anayemuona kuwa atafaa kuongoza kutokana na jinsi na yeye upeo wake unavyoona.
Ni kweli inashangaza kuona yule aliyekuwa anaonekana kukubalika na wengi kushindwa na mpinzani wake kushinda ila cha kuzingatia ni kutoamini kinachoandikwa/kusemwa katika vyombo vya habri bali matokeo rasmi ya jambo fulani.
Je, una lolote la kutuambia kuhusiana na hili. Kuwa huru kutuandikia maoni yako.
Chanzo: Telegraph, mitandao mbalimbali.
One Comment
Comments are closed.