Kampuni nyinhgi zinazofanya biashara ya simu janja zina desturi ya kutoa masasisho ya kila mwezi kwa lengo za kuzifanya rununu ziwe madhubuti lakini pia kurekebisha vitu ambavyo vimeonekana kuwa havipo sawa.
Samsung ni miongoni mwa kampuni ambazo zinatoa mara kwa mara masasisho kwenda kwenye simu janja zake kwa lengo za kuendelea kuzifanya ziwe salama zaidi. Mwezi ndio tumeuanza na tayari masasisho ya mwezi huu yalikuwa yameshatoka yakihusisha simu janja kadhaa za Samsung.
Samsung Galaxy S21, S21+, S21 Ultra na Z Flip 5G ni simu janja za kwanza kua kwenye msururu wa kupokea masasisho ya ulinzi kwa mwezi Juni 2021.
Kuna msema wa Kiingereza ambapo kwa tafsiri isyo rasmi ni “Kitu kizuri huanzia nyumbani” kwa maana ya kwamba masasisho yameonekana kwenye simu janja husika nchini Korea Kusini. Simu janja (S21, S21+ na S21 Ultra) ambazo zimepelekewa masasisho kwa namba maalum- G991NKSU3AUE8, G996NKSU3AUE8 na G998NKSU3AUE8.
Kwa upande wa Galaxy Z Flip 5 pia imepokea masasisho ya mwezi Juni 2021 kwa nchi za bara la Ulaya kujuisha Uhispania, Australia, Bulgaria, Italia, Ufaransa, Uingereza na nyinginezo kadhaa.
Kama unamiliki mojawapo ya simu hizo basi ukae mkao wa kula mwezi Juni kupokea masasisho ambayo daima huma ni muhimu kwa usalama na ufanisi wa kifaa chako cha kiganjani.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.