Umewahi kupanda ndege? Teknokona leo tunakuletea orodha ya Mashirika bora ya Ndege Duniani unayoweza kutumia katika safari zako. Kuna mashirika mengi ya ndege duniani na yamegawanyika katika makundi tofauti tofauti kama Mashirika ya ndege ya nchi, mashirika ya ndege ya kibiashara na ndege za kukodisha.
Aina za ndege zilizozoeleka katika usafirishaji wa abiria ni pamoja na Boeing 737, Boeing 747, Boeing 777, Airbus A320, Airbus A330 na nyingine nyingi. Vigezo vinavyotumika kupanga mtiririko wa ubora wa shirika la ndege kuanzia la kwanza mpaka la mwisho ni pamoja na wepesi we utaratibu wa kukata tiketi, Ukarimu wa wahudumu wa ndege, Ubora wa viti vya kukalia na Huduma za chakula ndani ya ndege. 10 Bora ya Mashirika Bora ya Ndege duniani ni:
- Qatar Airways: Shirika la ndege la Qatar ndio shirika la ndege linaloogoza kwa ubora duniani na limeshika nafasi hii mara 6 mpaka sasa tangu mwaka 2001. Shirika hili pia limejishindia tuzo zingine nyingi kwa mwaka 2021 ikiwemo tuzo ya Shirika bora la ndege kwenye daraja la biashara. Qatar ina ndege za abiria zaidi ya 204 zinazosafiri kwenda maeneo mbalimbali duniani na baadhi ya aina za ndege wanazotumia ni pamoja na Airbus A320-200, Boeing 787-8, Airbus A350-900 na Boeing 777-300ER.
- Singapore Airlines: Shirika hili la ndege limekuwa likichuana na Qatar katika kushika nafasi ya kwanza. Singapore Airlines ni moja kati ya mashirika ya ndege duniani yenye ndege nyingi za kusafirishia abiria kwenda maeneo mbalimbali. Shirika hili lina ndege takribani 145 ikwa imechanganya ndege aina ya Airbus na Boeing.
- ANA All Nippon Airways: Hili ni shirika la ndege lililopo nchini Japan linalofanya safari za ndani na nje ya nchi. Shirika hili nalo pia linaongoza katika mashirika bora ya ndege duniani na lina ndege takribani 216. Miongoni mwa ndege zinazomilikiwa na shirika hili ni Airbus 380 ambapo zipo
- Emirates: Hili ni shirika la ndege la nchi ya Emirates, Shirika hili linaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya ndege aina ya Airbus A380 ambapo zipo 115 zinazotumika kusafirisha abiria sehemu mbalimbali duniani. Emirates pia wamejishindia tuzo mbalimbali kwenye baadhi ya vipengele vya huduma wanazotoa ikiwemo tuzo ya Shirika la ndege la kimataifa lenye nyota tano.
No Comment! Be the first one.