Teknolojia za miguso na za kutambua sura za watu zimezidi kukua na kutumika katika maeneo ya kiusalama na sasa MasterCard wawekeza katika teknolojia ya kuwawezesha wateja wao kutokuwa na haja ya kuandika PIN pale wanapofanya malipo, sura zao ndio zitakuwa zinatumika. Wateja wa MasterCard wataweza kutumia picha za selfi kuthibitisha malipo.
Kampuni hiyo inatarajia hivi karibuni kuanza kufanya majaribio kwa takribani wateja 500 wa huduma hiyo. Majaribio hayo yatahusisha utumiaji wa taknolojia ya utambuzi wa watu kwa kutumia alama za vidole (fingerprint) au kwa kutumia sura ya mtumiaji (facial recognition).
Fikiria: Unalipita huduma kwenye mtandao kupitia huduma ya MasterCard…badala ya kutakiwa kutoa PIN spesheli ya manunuzi mtandaoni utaweza kupewa chaguo la kujipiga selfie na basi muhamala utafanyika.
Na ili kuepusha watu wanaoweza kuchukua picha za watu wengine na kuziwekesha mbele ya kamera ili kudanganyika mfumo huo wa malipo, MasterCard wameweka hali ambayo itamlazima mtu husika kufamba na kufumbua macho wakati anatazama kamera.
Mfumo unafanyaje kazi?
Picha inayopigwa inatumwa kama data katika mfumo wa namba siri. Hivyo mfumo salama wa kibenki utakuwa unaruhusu kutokana na mpangilio wa namba husika zinazotengenezwa na mitambo yao pale mtu anapopiga picha.
Wanategemea kuanza kusambaza teknolojia hiyo mara moja baada ya kuangalia mafanikio na changamoto katika hawa wateja mia 5 wanaowajaribishia katika utumiaji wa teknolojia hiyo.
No Comment! Be the first one.