Hatuongelei matangazo yale ya kawaida kama yale unayoyaona Facebook na Google wameyaweka katika mitandao yao. Hapa tunaongelea zile program zisizotakiwa ambazo zinachukua mamlaka katika vivinjari kama vile Google Chrome na Mozila firefox na kuonyesha matangazo mengi sana kipindi unapotembelea mitandao tofauti tofauti katika kompyuta yako.
Matangazo haya mara nyingine huwapeleka watu moja kwa moja katika maduka makubwa ya kimtandao kama vile Target, Walmart na Aliexpress, na mara nyingine matangazo hayo yanaweza kusababisha kuweka kwa programu chafu kwenye kompyuta yako pale unapoyabofya.
Jizuie Kupata Program Hizo Za Matangazo
Habari nzuri ni kwamba makampuni mengi ya teknolojia wameweka njia mbalimbali za kuzuia au njia za kiusalama katika software zao kwa mfano Google wana Safe Browsing ambayo inawasaidia watu wenye Chrome, Firefox au Safari kutoweza tembelea mitandao yenye tuhuma mbaya na kushusha ‘software’ mbali mbali bila kibali
Lakini kuna kitu kingine ambacho watu wanaweza fanya ili kujikinga wenyewe. Watu wenye kompyuta inawabidi watumie programu endeshaji (OS) ambazo ni mpya zaidi na kuboresha vivinjari vyao kwa kushusha matoleo mapya. Hali hii itasaidia kompyuta yako kwa ujumla kwa kuwa kila toleao jipya lina marekebisho ya kukulinda zaidi.
- Kuwa na uchaguzi juu ya kitu gani unashusha (unadownload) ni njia nyingine ya kujikinga.
- Kusoma vigezo na masharti ni vigumu ndio! lakini jitahidi kusoma inaweza kukusaidia kujua vitu vingi katika hiyo program au software kabla hata hujaanza kuitumia
- Kama linki au mtandao wowote unaonekana sio ya kawaida basi usishushe kitu chochote kutoka katika mtandao au linki hiyo.
- Kama katika kuweka programu (install) inakuwa inakupa matangazo mengi achana nayo au kuwa mwangalifu, epuka kubofya kwenye matangazo hayo.
Licha ya hayo yote ni vizuri kushusha programu au apps katika mitandao ambayo ni rasmi.
Jinsi Ya Kutoa Programu Hizo Za Matangazo
Chaguo lako la kwanza ni kushusha ‘software’ ambayo itakusaidia kuondoa hayo yote kwa ajili yako. Avast ni ya kuaminika na ya bure. Pia unaweza lipia ‘Software’ katika makampuni ya usalama kama vile Bitdefender, Symantec na Kaspersky.
Watumiaji wa Chrome katika windows wanaweza tumia ile software removal tool ya Google. Apple wameelezea njia juu ya kufuta programu hizo hata Windows nao walitoa maelezo juu ya watu kutoa program hizo wenyewe katika kompyuta zao.
No Comment! Be the first one.