Mtangazo, matangazo, matangazo…..! Pengine hili limeshazoeleka sana huko mitandaoni lakini katika yale maeneo ambayo mwanzo hatukuona matangazo yakionekana huwa tunashangaa kidogo na sasa ni kwenye Windows 11.
Repoti mbalimbali zilitoka watu wakilalamika kuwa wamekua wakipata matangazo kadha wa kadha katika eneo hilo la start katika kompyuta zao ambazo zinatumia Windows 11 kama programu endeshi.

Ki uhalisia ni ni kwmaba lile eneo tulikau tumelizoea likiwa halina matangazo kabisa na kwa sasa kama matangazo yanaonekana pale kwa baadhi ya watu itakua ni kero.
Do we really need to stuff OneDrive promos in the user session flyout? Anything for that sweet sweet KPI 😭 pic.twitter.com/ZsQGmkntDS
— Albacore (@thebookisclosed) November 6, 2022
Ukiachana na hayo ni kwamba kwa sasa makampuni mengi yanatafuta njia mbadala katika kuhakikisha kuwa yanapata mapato mengi zaidi na njia moja waponi kusambaza matangazo mengi kwa wingi katika maeneo ambayo kampuni inaona yanafaa.
Kwa sasa jambio hili liko katika majaribio na ni maeneo machache ambayo yamechaguliwa ili kuweza kufanya majaribio juu ya jambo hili.
Matangazo ni njia ya kawaida kabisa kwa makampuni ya kiteknolojia, pengine ndio njia kuu kwa mitandao ya kijamii mingi sana ya kujipatia mapato.
Lakini ni wazi kwamba kwa kipindi hiki makampuni yamekua yakihakikisha kuwa yanaongeza njia nyingine za kuhakikisha kuwa wanaonyesha matangazo mengi zaidi.
Tumeona kwa makampuni kama vile Apple na Netflix wakiongeza vipengele vya matangazo katika baadhi ya huduma zao.
Kufikia mwaka 2023 pengine rasmi hili linaweza likafanyika kwa kiasi kikubwa maana tayari imeshaongea na makampuni kadha wa kadha ambayo yataweza kurusha matangazo yao kupitia katika windows.
Kwa upande wangu naona eneo la ‘Start’ sio sahihi sana kurusha matangazo kwani wengi ambao wanaingia katika eneo hilo wanakua hawana mambo mengi ya kufanya, kwa mwingine inaweza ikawa ni kuzima kompyuta tuu.
Kumbuka kama mtu lengo lake ni kuzima kompyuta hata akiliona tangazo ni kwa kiasi kidogo sana anaweza akaachana na kuzima kompyuta na akaingia katika tangazo hilo.

Kwa sasa ni wazi kuwa matangazo hayaepukiki kabisa, maana kila kona katika mtandao tunakutana nayo na kwa kuanzia tuu kampuni ya Micrsoft imeanza kurusha matangazo hapo lakini inatangaza bidhaa zake kw asana kama vile One Drive n.k
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kuwa kuongezeka kwa matangazo ni jambo sahihi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.