Siku ya jana ilikuwa mbaya kwa watu wote wanaotegemea mtandao wa simu wa Tigo. Swali la msingi ni “Je ni nani anatakiwa kufidia faida za kiuchumi zilizopotea kutokana na kutokuwa na mawasiliano kwa wateja hao!”.
Hakuna ubishi ya kuwa taasisi inayosimamia sekta hii ya mawasiliano inatakiwa kuweka sheria kali na faini kubwa kwa mitandao ya simu pale matatizo yao yanapokiwa mara kwa mara, naamini hii itaongeza umakini katika kuboresha zaidi sekta hii.
Kuna nchi nyingi tuu za barani Afrika kama Naijeria, Uganda, Ghana na Rwanda ambapo vyombo vinavyosimamia sekta ya mawasiliano vimechukulia hatua makampuni ya simu mbalimbali kwa kutotoa huduma ya sifa zinazoitajika, hii ni pamoja na tatizo la mara kwa mara la mtandao. Nadhani mida umefika kwa ukali huu pia kuchukuliwa hapa kwetu, kwani vingenevyo kila baada ya muda tutakuwa tunaona matatizo haya ambayo kwa kweli yanaleta hasara kubwa sana katika jamii nzima.
Bila kuchukua hatua za haraka nadhani tuendelee kusubiri kuombwa msamaha kila jambo hili linapotokea.
Yapi mawazo yako?
No Comment! Be the first one.