Katika makampuni nguli ya kutengeneza na kuuza simu kwa sasa huwezi kuiacha Xiaomi, ambayo ni kampuni maarufu sana kutoka china.
Mara kadha wa kadha kampui imekua ikitoa simu ambazo zinaleta ushindani na chachu ya hali ya juu katika soko. Kwa sasa kampuni iko mbioni kutoa matoleo ya Xiaomi 13.
Matoleo haya yatatoka rasmi tarehe moja mwezi disemba wa mwaka 2022 na simu hizi zitakua ni muendelezo wa yale matoleo ya Xiaomi 13 mbayo yalitoka mwaka jana, 2021.
Matoleo Ta Xiaomi 13 Yatakua Ni
Xiaomi 13
Xiaomi 13 Pro
Japo vyanzo mbalimbali vinasema kuwa kampuni itatambulisha na toleo jipya la programu endeshi ya MIUI 14 huko nchini China.
Xiaomi wao wamejisifia kua vifaa hvyo vitakuja na vioo vya mfumo wa OLED huku vikiwa na basel ndogo sana (Basel ni umbali kitoka kwenye kioo mpaka kwenye jumba la simu).
Kingine ni kwamba inasemekana kuwa prosesa yake itakua ni ile ya Snapdragon 8 Gen 2, huku matoleo yote yatakua na uwezo wa Telephoto katika kamera zake.
Kwa sasa itakua ni ngumu kutaja sifa zake zote za undani kwa simu hizi mbili lakini ni Imani yangu tutazijua kwa undani kabisa siku ya uzinduzi wa simu hizi.
Kwa haraka haraka jumba la simu hii –kulingana na fununu—ni kwamba linafanana sana na lile la simu za matoleo ya iPhone.
Ni wazi kuwa kwa mwaka huwa zinatoka simu nyingi sana, na kwa dunia ya leo kuna washindani wengi sana katika soko la simu na ni wazi Xiaomi huwa ni moja kati ya simu inayofanya vizuri kiushindani na kimauzo.
BORESHO: Tarehe ya uzinduzi imesogezwa mbele mpaka kufikia disemba 11.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani matoleo haya mawili yataleta uhindani mkubwa kwa simu ambazo tayari zipo sokoni?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.