Tangu Julai Mosi ya mwaka huu nchini Tanzania matumizi ya nenosiri kwenye kadi mpya za simu yameanza kutumika katika namna moja ya kuweka usalama.
Kutokana na mabadiliko ambayo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kuyatoa kwa makampuni ya simu lakini pia kukabiliana na uhalifu wa kidijiti watumiaji wa simu za mkononi ambao wamenunua kadi mpya za simu katika miezi ya karibu hakika wamekutana na ulazima wa kuweka nenosiri kabla laini haijafunguka na kuweza kutumika.
Binafsi hivi karibuni nilinunua kadi mpya ya simu, Halotel na mbali na uwepo wa namba za PUK lakini pia ipo pia nenosiri kwenye kasha ambalo linawekwa kifaa hicho.

Je, inawezekana kuondoa nenosiri?
Jibu la swali hili nashindwa kutoa la moja kwa moja kama inawezekana au haiwezekani lakini kwa Halotel kitu hicho HAKIWEZEKANI kwani binafsi nilijaribu kuondoa nenosiri ili nikizima simu nikiwasha isidai kuweka tarakimu hizo nne lakini zoezi hilo halikuwezekana.

No Comment! Be the first one.