Mkurugenzi Mtendaji wa Microsoft |
Kampuni ya Microsoft baada ya kuingiza Windows 8 sokoni mwishoni mwa mwaka 2012 ilitegemea kuleta ushindani wa kweli na kukuza mauzo ya kompyuta na hasa ‘laptops’ ambayo yamekuwa yakishuka kutokana na ushindani wa tablets.
Lakini kwa uchunguzi na taarifa za mauzo ambazo zimetoka ni kuwa hadi sasa haijafanya vizuri kabisa sokoni kama wenyewe walivyotegemea. Na zaidi ya yote wakurugenzi mbalimbali wa makampuni ya kutengeneza kompyuta kama Asus, wameshatoa malalamamiko yako baada ya kuona wananafasi kubwa ya kufanya vibaya kimauzo.
Ingawa Windows 8 imekuwa ni bora zaidi katika utendaji wa kazi, ila ukweli ni kuwa Microsoft wameitengeneza wakiwa na wazo la laptop zilizo na vioo vya ‘multi-touch’, ikiwa ni kuruhusu kutumia kwa kutumia miguso ya vidole kwenye kioo. Na teknolojia ya vioo vya aina hii ni ghari hivyo imepelekea laptop nyingi za Windows 8 zilizotengenezwa na makampuni mbalimbali kuwa ghari sana kwa watumiaji waliozoea laptop za bei ya kawaida. Na zaidi ya yote kukua kwa umaarufu wa tablets kama iPads na zingine zimefanya watu wengi kipindi cha sikukuu hizi kununua tablets badala ya kompyuta mpya, wengi wameona ni bora kufanya ‘upgrade’ ya kompyuta zao zile za Windows 7 kwenda 8 badala ya kununua kompyuta mpya ambazo bei zake zipo juu sana.
Vitu hivi viwili pamoja na kuwa na mtazamo mpya kabisa kwa Windows 8, kuna changia kwa kiasi kikubwa kufanya vibaya kwa kompyuta za Windows 8. Watafiti wengi wanaona njia pekee ya kukuza mauzo hayo ni bei ya kompyuta/laptop hizi kushuka na kuwa angalau chini kidogo ya bei za iPad na ili hilo liwezekane basi gharama za utengenezaji lazima zishuke.
- Asilimia 4.5 tuu ya kompyuta zote zinazotumia Windows 8 zilizonunuliwa ni zenye teknolojia ya miguso (multi-touch).
- Tablet ya Surface kutoka Microsoft ambayo nayo inatumia Windows 8 nayo bado haijaleta mauzo ya kuleta mageuzi katika soko la tablets.
- Laptop nyingi zenye uwezo wa kuhimili Windows 7 tegemea Windows 8 kufanya kazi vizuri sana bila matatizo yeyote.
- Katika moja ya maboresho mazuri kutoka Windows 7 hadi 8 ni ufanisi wa haraka zaidi na muonekano bora zaidi wa Windows 8.
*Imeandika kwa Msaada wa The Verge, Bussiness Insider na mitandao mingine.
No Comment! Be the first one.