Nintendo ni moja kati ya makampuni makubwa kabisa katika ulimwengu wa magemu, licha ya kuwa na magemu mengi sana kampuni inasifika kwa gemu lake la Super Mario Bros ambalo pia linapatikana katika kifaa cha Nintendo Switch.
Nintendo Switch ni kama kwenye makampuni mengine tuu maana mara kwa mara huwa wanatoa taarifa au ripoti ambayo inaonyesha maendeleo ya kampuni kwa jamii.
Maendeleo hayo yanaweza yakawa katika mifumo mingi lakini mara kwa mara huwa tunajikita zaidi katika muenendo wa mapato.
Nintendo imetoa ripoti juu ya muazo yake ya kifaa cha Switch ambacho ni kipya zaidi na kwa kipindi cha mwaka mmoja (Aprili 2022 mpaka Machi 2023).
Namba hiyo bilioni moja (nakala 1,036,150,000) ni kwa upande wa hardware na software kote kwa mjumuisho licha ya vifaa (hardware) vya Switch kushuka kimauzo.
Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa namba hiyo itashuka zaidi maana gemu hilo halifanyi vizuri katika soko kama ilivyokua zamani.
Ukiachana na kushuka kwa magemu hayo bado ni kwamba kampuni ya Nintendo ina mpango wa kutoa magemu mengine mengi kupitia kifaa hiki cha Switch.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani kampuni itaendelea na kifaa hiki mpaka mwakani au itaachana nacho?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.