Meta ambayo inamiliki mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, WhatsApp n.k imelazimishwa kuuza kwa hasara kampuni yake ya Giphy kwa bei rahisi na kuwa katika sehemu ya hasara.
Kampuni ya Giphy inajulikana kwa umaarufu wake wa kutengeneza GIF za aina mbalimbali ambazo zinatumika katika mitandao mingi ya kijamii.
Kwa kampuni zote zinazotengeneza na kusambaza Gif duniani kampuni ya Giphy ndio inashikilia namba moja na inaongoza kuwa na Gif nyingi kuliko jukwaa lingine lolote.
Ukubwa wa Giphy ni kwamba kwa siku wanakutana na matafuto ya Gif zaidi ya bilioni 1.3. Hii ikiwa ni namba kubwa sana kwa siku.
Hasara inakuaja kwamba kampuni ya Meta iliinunua kampuni ya Giphy kwa dola za kimarekani milioni mia nne na sasa wamelazimika kuiuza kampuni hiyo kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 53.
Hii ikiwa ni hasara kubwa sana ambayo kampuni imeonekana kuipata na kampuni ambayo imenunua Giphy ni kampuni ya Shutterstock.
Wakati Meta inainunua kampuni ya Giphy wataalam wengi wa mambo walipinga na sababu ilikua iko wazi kwamba Meta itaipendelea mitandao yake ya kijamii na Gif hizo kuliko mitandao mingine ambayo ni pinzani.
Kumbuka Giphy ndio kampuni kubwa kuliko zote ambayo inasambaza Gif katika mitandao ya kijamii mingine hii inaonyesha moja kwa moja Meta ndio inaonekana imeshikilia mpini wa wa ushindani sio?
Mamlaka ambayo inasimamia usawa na ushindani wa masoko The Competition and Markets Authority (CMA) imeamuru Meta kuuza kampuni hiyo, na ndio ambacho kimefanyika.
Licha ya mwanzo wakati Meta inainunua Giphy iliahidi kwamba Gif hizo zitakua zinapatikana katika mitandao mingine yote ya kijamii lakini bado mamlaka na wataalam wa mambo waliona haiku sawa.
Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unaona hii ni sawa kwa kampuni ya Facebook kupokonywa tonge mdomoni? Ningependa kusikia kutoka kwako.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.