Kampuni ya Meta, wamiliki wa Facebook, Instagram na Whatsapp imetangaza rasmi kwamba itaondoa uwezo wa matumizi ya ujumbe mfupi yaani SMS kwenye app ya Messenger kwa watumiaji wa Android. Mabadiliko yataanza rasmi mnamo Septemba 28, 2023.
Hii inamaanisha kuwa watumiaji wa Android ambao wamekuwa wakitumia app ya Messenger kama kuu kwa ajili ya kupokea na kujibu ujumbe wa SMS hawataweza tena kufanya hivyo. Badala yake, watahitaji kuatumia app tofauti za usomaji wa SMS – zile zilizokuja na simu husika, kama vile Google Messages au Samsung Messages.
Meta haikutoa sababu ya mabadiliko hayo, lakini inawezekana ni kutokana na sababu kadhaa.
- Kwanza, matumizi ya ujumbe wa SMS yamekuwa yakipungua katika miaka ya hivi karibuni, kwani watu wamebadilika kwa kuwa wanatumia zaidi app za kisasa kama vile WhatsApp, Telegram, na Signal.
- Pili, Meta inaripotiwa inatafuta kuunganisha huduma zake za ujumbe, na hatua hii inaweza kuonekana kama njia ya kuboresha app ya Messenger. Kuna wanaoamini itafikia wakati utaweza kupokea na kujibu jumbe za Messenger ukiwa ndani ya app ya WhatsApp.
Soma habari na maujanja ya apps mbalimbali – Teknolojia/Apps
Mabadiliko haya yanaweza kuwa ya usumbufu kwa baadhi ya watumiaji wa Android, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa ujumbe wa SMS kwa kiasi kikubwa unapitwa na wakati. Tayari watu wanatumia apps nyingi nyingine za kisasa katika mawasiliano yao ya ujumbe wa maandishi.
No Comment! Be the first one.