Pengine kampuni mama ya Facebook, Meta inapitia magumu sana kuliko tunavyodhani. Licha ya kuandika kuhusiana na kupunguza wafanyakazi wake >>HAPA<< lakini bado wanaachana na baadhi ya bidhaa zake.
Bidhaa zote mbili –kutoka Meta– ni vifaa janja na hii ni tofauti kabisa na bidhaa zake zile za mtadaoni au huduma zake. Bidhaaa ambazo kampuni inaachana nazo……
……kabisa ni saa janja na kifaa maalum kwa ajili ya kupigia zile simu za video na kwa kiasi kikubwa kampuni ilitaka kuuzia kifaa hicho kwa makampuni na biashara zingine.
Vifaa hivyo vya video vinajulikana kama Portal ambavyo kwa sasa vimesitishwa kuzalishwa na kampuni kwa ajili ya wateja wa mwisho.
Na kulikua na saa janja ambayo ilipewa jina ambalo ni la utambulisho lakini sio rasmi la ‘Milan’ nayo uzalishaji umesitishwa.
Ni mara nyingi tumeona bidhaa za aina hii ambazo zinaanzishwaga mara nyingi na mitandao ya kijamii huwa zinakufa baada ya muda tuu.
Kingee kinachoshangaza ni kwa saa hizi maana hata bado zilikua hazijafika kabisa katika soko lakini kampuni imeamua kusitisha utengenezaji juu kwa juu.
Kampuni mpaka sasa haijatoa sababu za msingi juu ya kwanini bidhaa hizi mbili zitapotea katika soko, lakini ni wazi kuwa kampuni inapitia magumu kwa sasa.
Kingine ni kwamba mtandao ulitangaza kupunguza watu kazi pengine namba kubwa ya kazi hizo kwa wafanyakazi zimetoka katika vitego hivi vya bidhaa hizi? Japokua hili halina uhakika zaidi.
licha ya kuwa vifaa hivi havikufika sokoni, lakini pengine vingeweza kuleta ushawishi katika soko pengine hata kufanya vizuri. Ni wazi kuwa kwa kiasi fulani kampuni itakua imepata hasara.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unahisi ni sawa kwa kampuni kufikia katika hatua hizo ingawa vifaa bado havijafika sokoni?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.