Ni wazi kwamba mitandao mingi ya kijamii ambayo inamilikiwa na Meta (Facebook, Instagram na WhatsApp) ina mahusiano ya moja kwa moja.
Mfano mzuri ni kwamba unaweza kutuma status katika mtandao wa WhatsApp na ikaenda moja kwa moja katika mtandao wa Facebook ambayo yote inamilikiwa na Meta.
Kipegnele ambacho kinaenda kuzimwa ni uwezo wa kuchat na marafiki zako wa Facebook katika mtandao wa Instagram.
Kipengele hiki kitazimwa katikati ya mwezi wa kumi na mbili na baada ya muda huo kupita jambo hili litabaki kuwa ni historia tuu.
Kingine ni kwamba kama kuna mazungumzo ambayo yameshawahi fanyika katika huduma hii basi hakutakua na uwezo wa kujibu tena (read only).
Na vile vile mazungumzo hayo hayataenda katika eneo lolote la mazungumzo (inbox) la mtandao wowote –facebook au instagram.
Kumbuka uwezo huu ulitambulishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019 na umekua una faida nyingi sana maana umerahisisha maisha ya wengi.
Mpaka sasa Meta bado haijaweka wazi juu ya sababu za kwanini imeamua kuchukua hatua hii na wengi wanahusisha kua ni matakwa ya kisheria zinazoongoza mitandao.
Kila lenye mwanzo lazima liwe na mwisho, na huu utakua ndio mwisho wa huduma hii, ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hili umelipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.