Kuwa na nembo ya akaunti iliyothibishwa imekuwa kitu cha muhimu kwa wenye akaunti Facebook, Instagram jambo ambalo linaongeza uaminifu kwa wafuasi wao. Lakini sasa uwepo wa akili unde umeleta changamoto mbalimbali.
Ukiona akaunti ya mtu ima alama ya pata ya bluu hakika utaamini kuwa hii sio akaunti ya magumashi kwani nembo hiyo inalipiwa kila mwezi. Lakini sasa Meta imejikuta ikikabiliana na kesi mbalimbali kutokana na watu wenye “Akaunti zilizothibitishwa” kiasi kwamba wanapatikana na makosa mwisho wa siku wanalipa faini ya mamilioni ya dola.
Katika kuboresha usalama na kupambana na akaunti zisizo za kweli Meta imekuja na mtindo mpya wa kuhakikisha anayepewa nembo ya kwamba akaunti imethibishwa basi ni ya kweli. Meta imeamua sasa mtu anayeomba akaunti yake ithibisqhwe ni lazima upige picha kwa kamera ya mbele ili kuthibisha anayeomba ni binadamu. Mbali na hilo ni lazima mhusika awe na miaka 18+ na uwe na historia nzuri ya matumizi ya Facebook bila kutoka nje ya mstari.
Hatua hii itasaidia sana kuondoa akaunti za maroboti (zinazotumia akilili mnemba) na akaunti ikishathibitishwa basi nembo yake (pata ya bluu) itaonekana pia kwenye Marketplace, Dating na sehemu nyingine ambazo Facebook inatoa huduma. Kitu cha kuvutia kabisa ni kwamba mchakato huu ni BURE.
Vyyanzo: Engadget, mitandao mingine
No Comment! Be the first one.