Lazima utakuwa tayari unafahamu kuhusu mabadiliko ya gharama ya matumizi ya mawasiliano hasa hasa kwenye suala la intaneti data. Soma kwa undani hapa!
Mheshimiwa January Makamba, Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kupitia akaunti yake ya Twitter amesema wameshaiandikia barua TCRA (Chombo cha usimamiaji wa sekta ya mawasiliano) kuitaka ichukulie hatua makampuni ya simu kutokana na kitendo chao cha kubadilisha bei ghafla wiki iliyopita.
Hajaongea sana kwenye tweet hiyo, inayoonekana hapa;
Today, we’ve written to TCRA to ask for action using Electronic and Postal Communications Act (Tariffs Regulations). pic.twitter.com/cWA2LTuT1F
— January Makamba (@JMakamba) February 17, 2015
<
p style=”text-align: justify;”> Kwa kifupi sheria ya mawasiliano inasema hivi kwa tafsiri ya haraka haraka;
- -Kampuni ya simu inatakiwa iwasilishe bei zake kila baada ya robo mwaka (miezi mitatu) kwa TCRA.
- -Kampuni ya simu haitakiwi kutumia bei ambayo haijapitishwa na chombo cha usimamizi (TCRA)
- –Kila baada ya miezi mitatu lazima bei hizo zitangazwe kwenye vyombo vya habari kwa lugha ya kiswahili na kingereza
- -Mtandao mkubwa wa simu (yaani wenye nguvu – na hapa mitandao yote mitatu ya Airtel, Tigo na Vodacom inasifa hii) inabidi iwasilishe mapendekezo ya bei mpya si chini ya siku saba kabla ya bei hizo kutumika
- -Na baada ya hatua ya hapo juu na kukubaliwa na TCRA, kampuni hiyo kubwa ya simu inabidi itangaze bei hizo mpya kupitia vyombo vya habari kabla ya bei hizo kuanza kutumika
Ukipitia kwa undani vipengele hivyo nadhani kwa asilimia kubwa utagundua kuna ambavyo havikufuatwa.
Nimeongea DG wa @TCRA_Tz, Prof. Nkoma, kumuagiza azungumze na makampuni haya juu ya bei za bundles: ukubwa, ughafla, upamoja (mitandao yote)
— January Makamba (@JMakamba) February 13, 2015
Cha kujiuliza je watachukuliwa hatua gani? Kwani kwa kiasi kikubwa wamefanya mabadiliko ya haraka na bila kutupa sababu za uhakika kwa kilichotokea. Wapo wanaodai kilichofanyika ni ‘price fixing’, yaani kitendo cha wale wenye nguvu zaidi kibiashara kukaa pamoja na kuja na bei inayowapa faida zaidi. Kitendo hichi ni kinyume na sheria.
Makampuni ya simu hayapaswi kupanga au kuratibu kwa pamoja bei; tukigundua hilo limetokea ni ukiukwaji wa kanuni za ushindani wa soko.
— January Makamba (@JMakamba) February 13, 2015
<
p style=”text-align: justify;”>
Sheria ya udhibiti wa mawasiliano haitupi nguvu ya kupanga bei, isipokuwa interconnection fees. Ushindani wa bei unapaswa kushusha bei. 1/3
— January Makamba (@JMakamba) February 13, 2015
TUTAKUJULISHA MPAKA MWISHO WA JAMBO HILI. Endelea kusoma TeknoKona!
Soma pia – Sababu za Mabadiliko kwa Gharama za Huduma ya Intaneti
No Comment! Be the first one.