Kampuni inayokua kwa kasi sana, Xiaomi, ya nchini China imekuja na laptop za kisasa zinazoonekana kuja moja kwa moja kushindana kimauzo na laptop za MacBook Air zinazotengenezwa na kampuni ya Apple. Fahamu Laptop za Mi Notebook Air.
Xiaomi ni nini?
Kama ulikuwa ufahamu Xiaomi ni moja ya kampuni inayokua kwa kasi zaidi duniani. Walianza na utengenezaji wa simu janja lakini kwa sasa wanatengeneza vitu vingi zaidi hii ikiwa ni pamoja na TV, kamera na vifaa vingine vya elektroniki na sasa wameingia katika utengenezaji wa laptop.
Soma Pia – Xiaomi yauza simu Milioni 2 ktk Masaa 12, Rekodi ya Dunia ya Guinness Yawekwa
Inasemakana Xiaomi waliuza takribani simu milioni 70 kwa mwaka 2015. Ingawa bidhaa zake nyingi zinaanza kupatikana kwa soko la China tuu ila baada ya muda nyingine zinaweza nunulika mitandaoni na kutumwa kwa mataifa mengine nje ya China.
Laptop za Mi Notebook Air
Wametambulisha matoleo mawili ya laptop, za Mi Notebook Air…na kama unavyoona jina lake, linafanana na jina linalotumika kwa laptop maarufu zinazotengenezwa na Apple, MacBook Air. Hili pamoja na muonekano wa laptop hizo inaonekana ni wazi laptop hizi zinalenga kushindana na laptop za MacBook Air sokoni. Laptop za Xiaomi zote zinakuja na toleo la Windows 10
>Sifa & Tofauti zake
Toleo la takribani dola 540 za Kimarekani (Tsh Milioni 1.2 | Ksh 55,000/=)
- Laptop ya ukubwa wa inchi 12.5
- Prosesa ya Intel Core M3 (integrated graphics)
- RAM – GB 4
- Diski Uhifadhi – GB 128 SSD na nafasi nyingine ya kuongeza diski nyingine ya SSD
Toleo la takribani dola 750 za Kimarekani (Tsh Milioni 1.65 | Ksh 76,000/=)
- Ukubwa wa inchi 13
- Prosesa ya Intel Core i5
- RAM – GB 8 DDR4
- Diski Uhifadhi – GB 256 SSD na nafasi nyingine ya kuongeza diski nyingine ya SSD
- Pia kwa wapenda magemu inakuja na kadi ya NVIDIA GeForce 940MX
- Upana/Urefu – mm 306.9 x mm 210.9 na uzito wa kg 1.28
Pia zote zinakuja na teknolojia ya kuchajia ya kisasa inayotumika pia kwenye laptop za MacBook ifahamikayo kwa jina la type-C USB. Pia inakuja na maeneo mawili ya kuchomekea USB. Laptop zote zinafunikwa na jumba (body) ya chuma (metal).
…..VS MacBook Air
Kwa kiasi kikubwa kwa ubora wake wa kimuonekano na ata kiteknolojia na huku ukilinganisha na bei za laptop za Mi Notebook Air….MacBook Air zinaendelea kuwa kwenye upande wa laptop za bei ya juu. Kama kawaida yao, Xiaomi wanaonekana kujifunza mengi kutoka kwenye MacBook Air na kuja na laptop yenye ubora wa muonekano na sifa zingine nyingi kwa kiwango cha ata cha juu zaidi pale ukilinganisha na bei yake nafuu.

Lakini bado kuna maeneo kama vile ya utofauti wa programu endeshaji na ata suala la ukaaji wa chaji wa laptop za MacBook Air bado zinaonekana zitahimili ushindani huu kutoka Xiaomi…hasa hasa nje ya China.
Wizi wa ubunifu? – Inasemekana sheria za hakimiliki za masuala ya kimuonekano zipo tofauti nchini China ukilinganisha na nchi kama Marekani. Na walichofanya Xiaomi ni kitu kinachokubalika na akionekani kama ‘wizi’ au ‘uigaji’ kivile…
Upatikanaji?
Inasemekana laptop hizi zitaanza kupatikana rasmi tarehe 2 mwezi wa nane mwaka huu. Usitegemee kuziona kwa haraka katika maduka yetu kwa kuwa mfumo wa usambazaji wa bidhaa za Xiaomi bado haupo kwa mataifa mengi na hivyo upatikanaji wa bidhaa zake kwa mtu binafsi unaweza agiza moja kwa moja kupitia mtandao au kubahatika dukani kwa mfanyabiashara anayenunua vitu kutoka nchini China.
Soma Pia – Xiaomi yauza simu Milioni 2 ktk Masaa 12, Rekodi ya Dunia ya Guinness Yawekwa
Je wewe una maoni gani juu ya ujio wa laptop hizi kutoka kampuni ya Xiaomi?
Vyanzo: Mitandao Mbalimbali