Kompyuta aina ya MacBook Air ambazo zipo chini ya Apple (kampuni) mwaka 2018 inatimiza miaka 10 tangu hapo marehemu Steve Jobs alipoitambulisha kompyuta ya kwanza toleo la MacBook Air mwaka 2008 na kuifanya kompyuta hiyo kuwa maarufu tangu hapo na mpaka hivi leo.
Kwanini MacBook Air ni urithi kwa dunia aliouacha Jobs?
Kompyuta za wakati huo zilizokuwepo tayari sokoni mwaka 2008 kurudi nyuma karibu zote zilikuwa na sifa zinazofana; zilikuwa na wembamba wa karibu inchi moja, uzito wake ukiwa Kg 3.18, ukubwa wa vioo vya kompyuta hizo ulikuwa kati ya inchi 8-11 na nyingi kati ya kompyuta hizo hazikuwa na keyboard ambayo imejaa katika eneo lake.
Miaka 10 ya MacBook Air: Mwaka 2008 MacBook Air ilikuwa ikiuzwa kwa $1,799|Tsh. 4,047,750
Mageuzi yaliyokuja kufanywa na Jobs kwa kuleta MacBook Air kwa ulimwengu yalibadilisha kabisa taswira ya kompyuta kutokana na kompyuta hizo kuwa nyembamba sana Apple iliachana kuweka sehemu ya CD Drive, kutumia diski uhifadhi za SSD, kutumia vidole viwili kutembeza kipanya, kuwa na sehemu moja tu ya USB 2.0, shehemu ya kuchomeka DVI na kuwa na sehemu ya kuchomekea spika za nje.
Katika uzinduzi wa wa MacBook Air mwaka 2008 marehemu Steve Jobs aliitambulisha kompyuta hiyo kutoka kwenye bahasha nyembaba sana jambo ambalo liliwashangaza watazamaji waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wa MacBook Air.
Sony VAIO X505 (2004) ndio ilikuwa nyembaba zaidi kwa wakati huo mpaka pale MacBook ilipokuja mwaka 2008.
SIo miaka mingi sana iliyopita washindani wa Apple nao walipoanza kutengeza kompyuta ambazo zinafana kwa umbo na hata baadhi ya sifa za ndani za kompyuta hizo. Apple ilikataa kuunda upya MacBook Air ili kuweza kuleta ushindani na kompyuta kama vile Dell XPS 13 na badala yake ikatoa MacBook ya inchi 12, 13.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|