Mwaka 1976 mwezi April tarehe moja watu watatu Steve Jobs, Steve Wozniak na Ronard Wayne walianzisha kampuni ya Apple ambayo miaka arobaini baadaye imekuwa ni kampuni kubwa katika teknolojia.
Katika miaka 40 ya Apple yapo matukio mengi na mambo mengi ambayo yamefanyika lakini sio yote yanajulikana zaidi, makala hii itakuletea mambo ambayo hayajulikani saana kuhusu apple.
- Mjue Ronald Wayne ambaye ni mmoja ya waanzilishi wa kampuni ya Apple.
Ronald aliuza share zake za apple kwa dola za kimarekani 800 mda mfupi tu baada ya yeye na wenzie kuanzisha kampuni ya Apple, inasemekana kwamba alifanya hivyo baada ya kuhofia kwamba iwapo Apple wangeshindwa kibiashara basi mali zake zingebinafsishwa.
Wasichojua wengi kuhusu Ronald Wayne ni kwamba anajihusisha na mahusiano ya watu wa jinsia moja, na alimwambia habari hii Steve jobs wakati bado wakiwa waajiriwa kabla hawajaaanzisha kampuni ya Apple.
Ronald anasema hajutii kuuza hisa zake Apple wiki chache baada ya kuanzishwa, anadai kwamba aliyafanya maamuzi hayo kwa kutegemea taarifa aliyokuwa nayo kipindi kile . Yeye ndiye mbunifu wa logo ya kwanza kabisa ya Apple.
2. Steve Jobs aliuza gari lake ili aweze kutengeneza kompyuta ya kwanza ya Apple
Pesa ambazo ziligharamia utengenezwaji wa Kompyuta ya kwanza ya Apple ambayo ilikuwa inajulikana kama Apple computer 1 ama Apple 1 zilitokana na pesa zilizokusanywa baada ya Steve Jobs kuuza usafiri wake wa pekee wa VW mini bus na Steve Wozniak kuuza calculator yake ya HP-65
3. Kompyuta ya kwanza ya Apple ilichukua siku kumi tu
Baada ya kuwa na pesa kwa ajiri ya kutengeneza kompyuta iliwachukua Apple siku kumi kukamilisha kazi. Kompyuta hiyo ikauzwa kwa dola za kimarekani 666.66 Wozniak anasema hakuwa anajua chochote kuhusu mambo ya kishetani kuhusishwa na namba hiyo kwa wakati huo hivyo hiyo namba haina uhusiano wowote na imani za kishetani.
4. Steve Jobs aliwahi kushwa cheo akaamua kwenda kuanzisha kampuni nyingine.
Mwaka 1985 Steve Jobs alishushwa cheo cha umeneja na bodi ya wakurugenzi baada ya kutokea kugombea madaraka katiyake na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa wakati huo, Jobs akaondoka na baadhi ya wafanyakazi wakaanziasha kampuni ya NEXT.
Hata hivyo mkurugenzi mtendaji aliyesababishwa kuondoka kwa Jobs Apple alisababisha hisa kushuka na hivyo akaondolewa na baada ya muda akaajiriwa mtendaji mwingine ambaye alimrudisha Jobs Apple kwa kununua kampuni ya NEXT. Tukisheherekea miaka 40 ya Apple tujifunze kutoka kwa mwanzilishi wake Jobs ambaye hakukata tamaa aliposhushwa cheo katika kampuni yake.
5. Apple walishawahi kuwa na pesa nyingi kushinda serikali ya Marekani
Kwa kipindi kifupi mwaka 2011 Apple walikuwa wanahifadhi ya pesa kubwa hata kushinda hifadhi ya pesa ya Serikali ya Marekani, Hii ilitokana hasa na ukubwa wa madeni ya Marekani kwa wakati huo.
Yako mambo mengi ambayo hayajulikani kwa watu hasa watumiaji wa bidhaa za Apple hayo matano ni ni machache ambayo mimi ninmepata kuyafahamu, wakati tunasheherekea miaka 40 ya Apple naomba utuambie ni mambo gani ya Apple unahisi sisi hatuyajui?