Surface Duo ndio tabiti ya kwanza ya kujikunja (fold) kutoka kwao Microsoft na kwa mara ya kwanza kabisa ilikua imeachiwa mwaka 2020.
Kwa sasa ni wazi kabisa kwa Surface Duo imefikia mwisho wake kabisa na Microsoft wanaachana kabisa nayo.
Kinacho washangaza wengi ni kwamba kifaa hiko kilipata masasisho (update) mbili tuu za Android (OS).
Cha kushangaza kingine ni kwamba hayo yote ya kupata masasisho mawili tuu haijulikani ni kwanini imekua hivyo.
Kingine ni kwamba wataalam wa mambo wanadaia kwamba hata kampuni (Microsoft) itaachana na Surface Duo 2 pia.
Inaonekana dhahiri kwamba huu ni muendelezo tuu na hiyo ni baada ya ile ya kwanza kuachana nayo kabisa ikumbukwe kuwa Duo 2 ni ya mwaka 2021
Kuhusiana na Duo 2 ni kwamba yenyewe itakua ikipatiwa mifumo mipya ya OS na utaalam mwinigne mpaka kufikia 2024.
Hapa kinachofanyika ni kwamba kwa wale ambao tayari wana vifaa hivi wataendelea kutumia kama kawaida lakini wakae kwa kujua ….
…. Kwamba kwa kiasi kikubwa Microsoft kwa upande wao watakua hawatoa msaada wowote au matoleo mapya na masasisho ya Android ambayo yanahusiana na vifaa hvyo kufikia 2024.
Ni wazi kwamba Microsoft wenyewe hawajatoa bidhaa zinazohusiana na Surface Duo kwa muda mrefu mpaka sasa.
Hii inaonyesha kabisa kwamba muendelezo wa Surface Duo pengine hautaweza kufanikiwa kabisa na pengine hichi ndio kifo chake kabisa kwa ujumla.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je hili unalichukuliaje je wewe unahisi huu ndio mwisho wa vifaa hivyo? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.