Micromax ni moja ya kampuni kubwa zaidi pale linapokuja suala la simu na tableti janja nchini India. Kampuni hii ya wazawa imejikita katika kutengeneza bidhaa zenye kiwango cha kati na cha juu kidogo kwa bei nafuu ukilinganisha na makampuni mengine makubwa duniani kama vile Samsung na HTC.
Kampuni hii ya Micromax leo hii wametambulisha simu janja yao mpya ambayo imepata sifa ya kuwa simu janja nyembamba zaidi duniani kwa sasa. Simu hiyo inayotumia Android pia ni nyepesi sana ukilinganisha na simu kutoka kwa makampuni mengine zenye sifa kama ya simu hii.
Simu hiyo inayokuja na teknolojia ya hadi 4G/LTE katika mawasiliana ya data itakuwa inauzika kwa takribani Tsh 640,000/=.Kwa bei hii simu hii inakuwa moja ya simu za bei ghari sana kutengenezwa na kampuni hiyo ila wenyewe wamejitetea wakisema hii imetokana na wao kutumia vitu vya hali ya juu kama vile bodi kuwa la alumini (aluminium).
Katika kuitangaza simu hiyo kampuni hiyo imefanikiwa kuingia katika mkataba na moja wa wasanii wakubwa katika filamu za Hollywood, Bwana Hugh Michael Jackman anayesifika sana katika uigizaji wake wa filamu za X-Men.
Simu hiyo iliyopewa jina la Canvas Sliver 5 ina RAM ya GB 2 na ujazo/storage wa GB 16 na haina chagua la SD Card.
Sifa Kuu zingine za simu hiyo ni kama hivi;
Micromax Canvas Silver 5 | Sifa: |
---|---|
Kioo: | Inchi 4.8 cha AMOLED (cha mguso) |
Wembamba: | mm 5.1 |
Uzito: | gramu 97 |
Kamera: | MP 8 (Kamera ya nyuma); MP 5 (ya selfie) |
Betri: | 2000 mAh |
Programu Endeshaji: | Android Lollipop |
Tupe maoni yako na kumbuka kusambaza makala ya TeknoKona! Je unadhani simu za bei rahisi zinakuwaga na mvuto?
ni aina gani ya simu yenye uwezo mkubwa kwa kupiga picha hapa duniani