Kampuni ya Microsoft imetangaza kwamba kivinjari/kisakuzi (Browser) chake cha Microsoft Edge sasa kitapatikana katika mifumo ya Simu Janja za Android na iOS.
Microsoft Edge imekuwa ikitumika kama kivinjari katika mfumo wa Kompyuta wa Windows 10 na imekuwa na maboresho mazuri zaidi kuliko Internet Explorer.
Microsoft Edge ni mrithi wa Internet Explorer iliyokuwa ikitumika katika mfumo endeshi wa Windows kwa kipindi chote cha nyuma.
Microsoft imethibitisha Edge itapatikana katika mifumo ya Android na iOS na kwa sasa kuna toleo la Beta ambapo kufikia mpaka mwishoni mwa mwaka watakuwa wametoa toleo kamili kwa wote.