Microsoft kwa kifua mbele kabisa imeweka wazi kwamba ilikua na mpango wa kuuza mtandao wake wa Bing kwa Apple lakini Google wao ndio walisababisha dili hilo lisifanikiwe.
Licha ya kuwa ni makampuni makubwa (Apple, Google Na Microsoft) sana bado yanauziana bidhaa na huduma mbalimbali baina yao.
Miaka kadhaa nyuma niliandika kuhusiana na Google kuwalipa mamilioni ya pesa Apple ili kufanya tuu Google iwe ndio kituo kikuu cha matafuto katika vifaa vya Apple..Soma zaidi >>>HAPA<<< na >>>HAPA<<<
Hii inaonyesha kabisa kwamba Apple na Google kwa kipindi cha muda mrefu wana makubaliano yao ambapo Google wamelazimika kuwalipa Apple kwa ajili ya huduma.
Microsoft na wao walikuja na dili kama hili na hata kama ikibidi wangeweza kuuza Bing kwa Apple lakini haikufanikiwa kisa Google.
Kingine ambacho kiliwashangaza wadau wengi ni kwamba Microsoft yeye alikuwa tayari ameandaa dau kubwa ili kuwapa Apple kuliko Google walivyofanya.
Baada ya hili kushindikana wataalam wa mambo wakakubaliana tuu kwamba kuna mambo mengi baina ya wawili hao ukiachana na dili hilo tuu.
Ni wazi kwamba mpaka sasa Apple inaingiza pesa nyingi sana kupitia katika kampuni ya Google na hii ni kwa kupitia huduma yake ya kutafuta (search engine)
Ningependa kusikia kutoka kwako`niandikie hapoc chini katika eneo la comment je unadhani Apple wangeinunua Bing kungekua na mabadiliko yoyote?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.