Microsoft ni kampuni kubwa sana ambayo inajihusisha na mambo mazima ya kiteknolojia, mara kwa mara imekua inanunua makampuni mengi na sasa ni zamu ya Fungible.
Fungible ni kampuni changa ambayo kwenye soko ina miaka 6 tuu, lakini imenunuliwa na Microsoft kwa kiasi cha dola milioni 190 za kimarekani.
Fungible ni kampuni ambayo inajihusisha na maswala mazima ya usindikaji wa data (data processing unit) au kwa kifupi DPU.
Microsoft yenyewe inasema kwamba itatumia teknolojia hii kwa kuiingiza katika teknolojia zake zingine katika ubunifu na hata kuendeleza mifumo mingine.
Kwa haraka haraka ni kwamba DPU ni mfumo wa kifaa ambao kazi yake kubwa ni kushughulikia kazi fulani ambayo imepangiwa.
Hii yote inafanyika katika kuhakikisha kuwa CPU na GPU zinapunguziwa kazi kwa kiasi fulani ili zijikite sana katika kazi kubwa kubwa.
Fungible ilizalishwa mwaka 2016 na mwanzilishi wake bwana Bertrand Serlet ambae ni injinia wa zamani wa Apple katika kitengo cha Software.
Kingine ni kwamba inasemekana teknolojia hii inaweza ikawa inatumika katika kuiongezea nguvu Azure na kwa haraka haraka ni kwamba timu ya Fungible itajiunga na timu ya Microsoft katika kufanikisha yote hayo
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani kampuni hii Microsoft itaitumia katika Nyanja gani katika kampuni hilo.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.