Akili bandia ni nyingi sana siku hizi na huwa zinatofautiana baina ya moja na nyingine. Hali hii inaonyesha dhahiri kwamba teknolojia inazidi kukua siku hizi na hata Microsoft wao wameamua kuja na Copilot.
Copilot sio kwamba itakua inatumiaka na App zote zinazomilikiwa na Microsoft la-ha-sha, bali yenyewe itakua imejikita katika App zote za Microsoft Office 365.
Kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa inasaidia watumiaji wa App hizo katika uandaaji wa nyaraka, barua pepe, uwasilishaji (presentation) na mambo mengine mengi.
Sasa unaweza ukajiuliza kwamba hayo yote yanafanyikaje? Jibu ni kwamba kuna akili ya bandia (Artificial Inteligency/AI) ambayo inafanya haya yote kuwezekana.
Mfumo wa Copilot ambao unatumika ni GPT-4 kutoka katika OpenAI. Kumbuka kupitia OpenAI ndio dunia imegahamu teknolojia ya ChatGPT, Soma zaidi >>HAPA<<
Discover a new way of working with Microsoft 365 Copilot—next-generation AI capabilities embedded in the Microsoft 365 apps you use every day. Learn more: https://t.co/fqTtN1tRVQ pic.twitter.com/gNjCQfGkdz
— Microsoft 365 (@Microsoft365) March 16, 2023
Lengo lingine la Copilot ni kwamba litakua ndani ya App za Microsoft 365 kama msaidizi tuu na itakua ikionekana pembeni kama ‘Chatbot’ ambayo watumiaji watakua wanaiamuru kufanya mambo mbalimbali.
Mambo hayo yatakua yanafanyika ni kama vile kuongezea maeneno katika nyaraka, kuandaa uwasilishaji (presentation) kutoka katika faili (File) la Word na kuweza kubadilisha mafaili mengine kuwa katika mfumo mwingine.
“Hii inafanya kazi sambamba kabisa na wewe, iko ndani ya mamilioni ya App ambazo watu wanazitumia kila siku: Word, Excel, PowerPoint, Outlook, Teams, na nyingine nyingi” —- alisema mkuu wa Microsoft 365, Jared Spataro
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Unadhani kwa jinsi teknolojia inavyokwenda kwa kasi kiasi hiki si kuna kipindi kitafika binadamu atakua hana cha kufanya katika kompyuta licha ya kuiamuru tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.