Kampuni nguli ya kiteknolojia ya Microsoft imekuaja na taarifa mbaya amabayo inahusiana na kupunguza wafanyakazi wake huko nchini urusi.
Hii sio kampuni ya kwanza kupunguza wafanyakazi wake, hii inamaana kuwa kampuni hiyo inajiunga na makampuni mengine katika kupunguza wafanyakazi.
Kwanza kabisa iliaanza kusimamisha uuzaji wa bidhaa na utoaji wa baadhi ya huduma mwezi machi mwaka huu.
Licha ya kuwa wanajipunguza sana katika nchi hiyo, wameweka wazi kuwa bado watakizi matakwa ya kimkataba baina yao na wateja wao —-hata kama wakiondoka kabisa—
Kwa upande wa Microsoft wao wanasema wamechukua hatua hii kwa sababu ya sababu za kiuchumi baina yao na nchi hiyo.
Ikumbukwe kuwa nchi nyingi tuu kama vile Apple, Nike, Dell, Adidas na mengine mengi nayo yalipunguza watu au kutoka kabisa katika nchi ya urusi.
Asilimia kubwa–kwa sasa– ya makampuni haya huwa yanashindwa kuendeleza biashara na utoaji huduma wake nchi humo kwa sababu ya vita kati ya urusi na Ukraine.
Nigependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini kwenye uwanja wa comment, hali hii unaionaje maana idadi kubwa ya makampuni yanajitoa katika nchi ya urusi.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.