Visual Studio inamilikiwa na kampuni ya Microsoft na imekua ikipatikana katika Os mbali mbali lakani kwa sasa inaonekana dhahiri kwamba inapumzishwa dhahiri katika Mac.
Visual Studio kazi yake kubwa ni mfumo unaokwenda kwa jina la Integrated Development Environment (IDE) ambao umeandaliwa na kampuni ya Microsoft
Kazi yake kubwa ikiwa ni kuandaa/kutengeneza GUI (Graphical User Interface), console, web apps, mobile apps, cloud, shuduma zingine za kimtandao n.k
Ni wazi kwamba huduma hii ilikua inawasaidia sana wazalishaji wa mambo mbali mbali kama vile Apps n.k
Kinachopelekea mpaka kampuni kuachana na Visual Studio kwa ajili ya Mac ni kwamba kampuni imejitahidi sana katika kuhakikisha kuwa inafanikisha ile ya Mac kuendana sambamba na ile ya Windows.
Kwa harakahara hata katika kipindi cha mwanzo 2022, kipindi ambapo husuma hii ilikua inatambulishwa ilichelewa miezi sita baada ya kutoka ili mradi kurekebisha baadhi ya kasoro za kiutendaji kazi n.k
Microsoft yenyewe imesema kwamba kuanzia leo yenyewe inawekeza nguvu zake nyingi katika kuhakikisha kwamba Visual Studio na VS Code zinakua zinaingiliana.
Hakuna framework,runtime au lugha mpya ambayo itakua imeongezwa katika Visual Studio ya Mac na hii ni kwa kipindi cha miezi 12.
Kitakachokua kinafanyika ni kwamba Microsoft watakua wakitoa masasisho (updates) za muhimu kama vile bug fixes, ishu za kiusalama n.k
Lakini pia upendeleo huu utadumu kwa mwaka mmoja kwa maana ya kwamba mpaka kufikia agosti 31,2024
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je huduma hii kusitishwa katika Mac na kuendelea katika Windows ni jambo jema?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.