Kila lenye mwanzo linakuaga na mwisho sio? Kwa sasa ni zamu ya kivinjari ambacho kilijipatia umaarufu sana miaka ya nyuma yaani internet explorer.
Internet explorer ilianza kutumika mwaka 1995 na kikijipatia umaarufu kwa kasi na kuwa ndio kivinjari pendwa kwa watu wengi.
Miaka inabadilika, teknolojia inazidi kukua kwa kasi, mambo yanabadilika na hatimaye kampuni ya Microsoft imeamua ikizike tuu kivinjari hiko maana kimeshapata mrithi siku nyingi tuu.
Internet Explorer ilianza kupunguzwa katika baadhi ya vifaa kulingana na program endeshi zinazotumika (windows) mfano kivinjari hiki katika Windows za juu kilikuwepo lakini ilikua ukikichagua kinakupeleka katika edge.
Mrithi wa Inetrnet Explorer ni kivinjari cha Edge ambacho ndio kitakachokua kinatumika katika vifaa vyote vya Microsoft kwa sasa
Tumeshaandika sana kuhusina ana kivinjari hiki unaweza soma kwa kuingia >>HAPA<<
Kwa sasa kuna vivinjari vya aina nyingi sana hivyo kuna ushindani mkubwa sana baina ya hivyo, mfano kivinjari kama cha google Chrome kina ushindani mkubwa sana na hichi cha edge maana vyote ni vikubwa.
Lakini ukifikiria kwa umakani ni kwamba hakuna kilichoharibika sababu ukifuatilia kwa umakini ni kwamba kila kitu ambacho ulikua unakipata kupitia kivinjari cha internet explorer kwa sasa unaweza ukakipata zaidi katika kivinjari cha Edge.
Kwa muda tuu Microsoft waliweka wazi dhima yao ya kukituliza kivinjari hiki ila kwa muda hawakukifuta kabisa katika vifaa vyake vyote na sasa ndio wameamua kufanya hivyo.
Kumbuka Edge ilianzishwa mwaka 2015 kama mrithi wa Explorer lakini bado vivinjari vyote viwili vilikua vinapatikana katika kifaa kimoja na vyote vilikua vinafanya kazi.
Mpaka kufikia mwezi juni hautakua na uwezo wa kuona chochote ambacho ni App/folder katika kompyuta au kifaa chako chenye neno la internet explorer.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani ni sawa kumfuta kabisa mkongwe huyu wa vivinjari?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.