Microsoft na janga la CrowdStrike, Microsoft waleta programu ya urejeshaji inayolenga kusaidia wasimamizi wa mifumo ya TEHAMA (IT) ili kutengeneza kompyuta za Windows zilizoharibiwa na sasisho batili la CrowdStrike lililosababisha zaidi ya vifaa milioni 8.5 vya Windows kushindwa kufanya kazi kuanzia Ijumaa iliyopita.
Programu hii itakayohitaji kuweka kwenye USB, na kuwa kwenye kompyuta wakati inawashwa, programu hii itawaruhusu wasimamizi wa mifumo ya TEHAMA kufanya maboresho ya mfumo uendeshaji wa Windows kuweza kutatua tatizo lililosababishwa na sasisho la CrowdStrike.
Ingawa CrowdStrike imetoa sasisho la kurekebisha programu yake iliyosababisha mamilioni ya hitilafu za Blue Screen of Death, si kompyuta zote zinazoweza kupokea sasisho hilo moja kwa moja. Baadhi ya wasimamizi wa IT wameripoti kwamba kuwasha tena PC mara kadhaa kunaweza kupokea sasisho hilo muhimu, lakini kwa wengine njia pekee ni kuwasha kwa mkono katika Hali Salama na kufuta faili ya sasisho la CrowdStrike linalosumbua.
Utaratibu na programu hiyo inapatikana kupitia – https://techcommunity.microsoft.com/t5/intune-customer-success/new-recovery-tool-to-help-with-crowdstrike-issue-impacting/ba-p/4196959
No Comment! Be the first one.